0




Ligi daraja la nne,ligi hii limezaminiwa na mbunge wa jimbo la Liwale,mh, Zuberi Kuchauka (Kuchauka cup 2016) leo ikiwa octoba 24 limeanza kutimua vumbi katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika mchezo wa ufunguzi kulikuwa na mchezo kati ya timu New generation dhidi ya Nangando fc katika mchezo huo New generation imeibuka na ushindi wa magoli 3-0.

 Magoli ya timu ya New generation yalipachikwa na Reheman Mtipa namo dakika ya 20 na Omari Matwiko aliweza kutikisa nyavu dakika ya 41 na dakika ya 88 Reheman Mtipa walipigilia goli la tatu.

Octoba 25 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya polisi fc vs Lingowele fc nimezungumza na kocha wa timu ya polisi fc, Karimu Libena amejigamba kama mchezo huo atapata point 3 kutoka kwa timu ya Likongowele fc

 SAUTI ZA MAKOCHA WALIPOELEZEA JUU YA MCHEZO WA UFUNGUZI

Post a Comment

 
Top