Taarifa
hii imetokea mianzini Arusha ambapo ndani ya nyumba aliyokuwa anaishi
Christopher Akoonay baada ya kubomolewa wakati wa zoezi la upanuzi wa
barabara na kikubwa kilichojitokeza ni mifuko ya plastiki iliyosheheni
mamilioni ya fedha ambayo ilikuwa imechimbiwa chini ya ardhi .
Imeelezwa
kuwa wapita njia na wakazi wa eneo hilo walipata neema ya kuokota fedha
baada ya trekta lililokuwa likichimba barabara kuzichimbuwa na zikawa
zimesambaa, lakini pia kuligeuka kilio kwa mmiliki wa hazina hiyo
Christopher Akoonay.
Siku ya
tukio, Akoonaay alikuwa yuko kwenye shuguli zake za kuwapelekea maziwa
wateja wake ndipo watengeneza barabara walipofika kutengeneza barabara
na kuanza kuichimba njia hiyo.
Christopher Akoonay ambaye amekuwa
akizitunza pesa hizo chini ya ardhi tangu mwaka 2014 amesema alikuwa
akiweka shilingi laki saba kila mwezi.
Gazeti la
Habari Leo limeripoti kuwa nyumba ya Akoonaay ni miongoni mwa zile
zilizobomolewa na ni baada ya wamiliki wake, kugoma kuzibomoa wenyewe
ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.
Post a Comment