WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi
kujitokeza kuwekeza mkoani Dodoma na serikali imejipanga kutoa ardhi na
kupunguza urasimu katika utoaji wa leseni.
Pia
alisema serikali inaunga mkono juhudi za wawekezaji katika sekta ya
viwanda na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa lengo la kukuza uchumi wa
taifa sambamba na kutekeleza azma yake ya kuendeleza viwanda nchini ili
taifa liweze kupiga hatua na kufikia uchumi wa kati.
Waziri
Mkuu, Majaliwa alisema hayo jana wakati alipotembelea kiwanda cha
kutengeneza magodoro cha Dodoma Asili cha mjini hapa na Kiwanda cha
Premalt Limited.
Waziri
Mkuu alisema serikali imefungua milango kwa wawekezaji wanaotaka
kujenga viwanda, nyumba za kuishi, kukodisha kama ofisi masoko makubwa,
maeneo ya bustani ya kupumzika na uwekezaji mwingine na serikali
itawaunga mkono.
“Ni
jukumu lenu Watanzania kuja kuwekeza Dodoma milango iko wazi. Serikali
hii itawaunga mkono wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza Dodoma, wale
wanaofikiria serikali haina nia njema na wafanyabiashara wajue
hatuhitaji kuweka siasa sana kwenye utendaji,” alisema Majaliwa.
Alisema
serikali inawapenda sana wafanyabiashara imejipanga vizuri katika kutoa
ardhi na kupunguza urasimu katika utoaji wa leseni.
“Hatutaki
kuweka siasa sana kwenye utendaji, sehemu kubwa ya ahadi ya Rais John
Mgufulini kuhakikisha wananchi wanapata tija ya kuhudumiwa na serikali
yake tatizo kubwa siasa imewekwa mbele sana,” aliongeza.
Alisema
Dodoma Asili ni kiwanda chenye kuzalisha magodoro yaliyo bora yenye
heshima na kuwataka watumishi wanaohamia Dodoma wasihame na magodoro
kwani Dodoma kuna kiwanda chenye ubora.
“Watumishi wanaokuja Dodoma hawana haja ya kuhama na magodoro,” alisema Majaliwa aliyehamia mjini hapa mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi
wa kiwanda hicho, Haidary Gulamali alisema kati ya wafanyakazi 150
walioajiriwa kiwandani hapo, 147 ni Watanzania na watatu ni wataalamu
ambao ni raia wa kigeni. Alisema magodoro ya kiwanda hicho yamekuwa na
soko zuri kutokana na ubora wake.
Alisema
pia anakusudia kuanzisha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta ya alizeti
ambacho kitakuwa na uwezo wa kukamua tani 100 kwa siku, ambapo kwa mwezi
zitakamuliwa tani 3,000. Alisema mradi huo mpya unatarajia kugharimu
kiasi cha Sh bilioni nne.
Katika
kiwanda ya kuzalisha unga wa kutengenezea gypsum kinachomilikiwa na
mwekezaji kutoka India, Arnod Chandra, Waziri Mkuu alisema serikali
itaangalia jinsi ya kuweka kodi kwenye bidhaa hiyo inayoingia kutoka nje
ya nchi ambayo haitozwi kodi.
|
Post a Comment