0
Simanjiro. Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Zephania Chaula amewasweka mahabusu madiwani wawili wa CCM.

Chaula amewaweka ndani madiwani hao akiwamo wa Kata ya Emboreet, Christopher Ole Kuya na wa Viti Maalumu, Diana Kuluo kwa madai ya kuvunja ofisi ya Kijiji cha Emboreet na kushinikiza wananchi kuandamana ili kumpinga mwenyekiti wa kijiji hicho.

Chaula alitoa amri ya kukamatwa kwa madiwani hao baada ya kuona wanaongoza kuharibu usalama kwenye eneo hilo.

Alisema madiwani hao waliwaongoza baadhi ya wanakijiji kuvunja ofisi ili kumshinikiza mwenyekiti wa kijiji hicho, John Olendikoni kujiuzulu na kusababisha waandamane kumpinga.

Akizungumza baada ya kuachiwa kwenye Kituo cha Polisi Orkesumet, Ole Kuya alisema hawakuwashinikiza wananchi kuandamana ili kumkataa mwenyekiti na kuvunja ofisi ya kijiji.

Post a Comment

 
Top