0

Mgeni rasmi Mr.Scott Allaw Plawck kwenye mahafali ya 8 ya kidato cha nne 2016 katika shule ya sekondari Nicodemus Banduka iliyopo kata ya Mbaya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nicodemus Banduka,Mohamedi Serafi akizungumza na wazazi,walenzi pamoja na wadau mbalimbali kwenye mahafali ya 8 ya kidato cha nne mwaka 2016
Akizungumza na wanafunzi,wazazi,walezi pamoja na wageni waalikwa katika mahafali ya 8 ya kidato nne - 2016,Mkuu wa shule mwalimu Mohamedi Serafi amesema tangu kuanzishwa kwa shule ya Nicodemus Banduka mwaka 2009 licha ya kuwa na changamoto lakini kuna mafanyikio ikiwa baadhi ya wanafunzi kuendelea na masomo ya kidato cha tano,vyuo vya uwalimu na vyuo vikuu mbalimbali.

Mafanyikio hayo yalisemwa octoba 22, 2016 Katika mahafali shuleni hapo, idadi ya wanafunzi walionza walikuwa 89 ikiwa wavulana 50 na wasichana 39 lakini mpaka wanahitimu idadi ya wanafunzi wanaohitimu ni 38 tu ikiwa wavulana 14 na wasichana 24 sawa na 44%.

Mwalimu Serafi alibainisha sababu zilizopelekea wanafunzi kushindwa kuhitimu ikiwa utoro sugu,wasichana kushika mimba,umasikini wa kipato wa kipato katika familia na wazazi kutojua thamani ya elimu.
Shule hiyo ilifunguliwa rasmi machi 17, 2009 ikiwa wanafunzi 89,wavulana 69 na wasichana 20,mwalimu mmoja ikiwana na madarasa mawili,nyumba ya mwalimu mmoja na sasa shule ina jumla ya wanafunzi 240 ikiwa wavulana 111 na wasichana 129,madarasa 8,vyoo matundu 8,maabara 1,bweni mmoja pia kuna jumla ya walimu 15,nyumba za walimu 5.

Shule hiyo licha ya kuwa na fanyikio lakini kuna changamoto nyingi ikiwa ukosefu wa vitanda,magodoro,maji safi,umeme,uzio,ukosefu wa chakula cha mchana kutokana na wanafunzi wengi kutoka mbali na kuja kuhudhulia masomo na uhaba wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia na uchakavu wa vyoo vya wanafunzi ambavyo vinatarisha maisha yao.

Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Liwale,Mary Ding'ohi alisema shule ya sekondari Banduka kupitia ofisi ya maendeleo ya jamii imechaguliwa shule hiyo kuwa ya mfano kwa kuanzisha club ya Ukimwi ambayo itakuwa endelevu.

Ding'ohia alisema kupitia ofisi ya idara yake itatoa kiasi cha shilingi 200,000 kwa ajili ya kuisaidia club ya Ukimwi kwa lengo la kupambana na ambukizi mapya na kufikia asilimia 0 (0%) na hakuna mtu atakaye nyanyapaliwa.

Katika hatua nyingine,mgeni rasmi katika mahafali hiyo ni Mr.Scott Allaw Plawck aliahidi kuzitatua baadhi ya changamoto kadhaa ainishwa katika hutuba yake. 

"Nilikiwa mdau mmoja wapo mpenda maendeleo nitasaidia kuwachimbia kisima kimoja nikishirikiana na diwani na idara ya maji pamoja na hilo pia nitatoa shilingi 100,000 kwa ajili ya kuiunga mkono club ya Ukimwi"  Alisema Scott.
 
Scott aliushuru uwongozi wa shule pamoja na wananchi kwa kumpa nafasi ya kuongea na wananchi kwani kitendo hicho kimemfurahisha sana kwakuwa yeye amekuja hapa nchini kwa kufanya kazi ya kimaendeleo akishirikiana na wananchi pia alisisitiza upandaji wa miti.
Wahitimu wa kidato cha nne 2016 wakisikiliza kwa umakini maelezo muhimu ya kuwatia moyo ili kuweza kufanya vizuri kwenye masomo yao 
Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Liwale,Mary Ding'ohi (kushoto) akiwa na mkuu wa shule ya sekondari Nicodemus Banduka
Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Liwale,Mary Ding'ohi akizungumza na wazazi,walenzi na wanafunzi kuhusiana na mashuala ya ukimwi na kuwataka wazazi kutambua thamani ya elimu ikiwa ya chekechea ikiwa ni muhimu sana kwa watoto wadogo.

 wazazi,walenzi pamoja na wadau mbalimbali walioudhulia kwenye mahafali ya 8 ya kidato cha nne 2016 katika shule ya sekondari Nicodemus Banduka.
wazazi,walenzi pamoja na wadau mbalimbali walioudhulia kwenye mahafali ya 8 ya kidato cha nne 2016 katika shule ya sekondari Nicodemus Banduka.
 wazazi,walenzi pamoja na wadau mbalimbali walioudhulia kwenye mahafali ya 8 ya kidato cha nne 2016 katika shule ya sekondari Nicodemus Banduka.
Mgeni rasmi akizunguza na wazazi,walenzi pamoja na wadau mbalimbali walioudhulia kwenye mahafali ya 8 ya kidato cha nne mwka 2016 katika shule ya sekondari Nicodemus Banduka.

 Hatua ya ugawaji wa vyeti maalumu pamoja vyeti vya uthibisho wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2016


 

Post a Comment

 
Top