Kwenye vitu ambavyo inawezekana hukua ukifahamu au kufikiria kama kuna
uwezekano wa kuwepo ni pamoja na hii issue ya upatikanaji wa mafuta aina
ya Diesel kwenye visima vya maji Mkoani Songwe.
Waziri wa Mazingira na Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe January
Makamba kwenye ziara yake ya mazingira amefanikiwa kufika katika mji wa
Mloo ulioko kwenye mkoa wa Songwe na kupokea taarifa ya mazingira ya
Mkoa ambayo imebainisha tatizo la uwepo wa mafuta ya Diesel kwenye
visima vya maji na kuelezwa kuwa mafuta hayo siyo mafuta ghafi
yanayotakiwa kupatikana ardhini.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa uvamizi wa shughuli za binadamu katika
vyanzo vya maji inatishia uhai wa vyanzo hivyo,Waziri Makamba ameahidi
kusaidia upatikanaji wa wataalamu ili kuweza kutambua chanzo cha tatizo
hilo la uwepo wa mafuta katika visima vya maji na kutambua njia sahihi
za kukabiliana na tatizo hilo.
Vilevile Waziri Makamba amefika katika Wilaya ya Ileje ambapo pia
amepokea taarifa ya Mazingira ya Wilaya na kupongeza juhudi kubwa za
wilaya ya Ileje katika utunzaji wa mazingira hasa eneo kubwa la misitu
uliopo katika lililopo katika Wilaya hiyona kuahidi pia kuzisaidia
Halmashauri za Wilaya na Vijiji namna sahihi na bora zaidi ya kuandaa
sheria ndogo za mazingira ili kukabiliana na changamoto za uharibifu wa
Mazingira.
Post a Comment