Mfumuko nchini Nigeria huenda umeathiri kampuni ya Dangote Group inayomilikiwa na mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote.
Kampuni hiyo imeripotiwa kuwafuta kazi wafanyikazi 48 wakiwemo wataalam 36 wa kigeni na raia 12 wa Nigeria.
Ripoti
zinasema kuwa hatua hiyo inatokana na gharama ya juu ya kufanya
biashara katika taifa hilo na kampuni hiyo imeshindwa kupata fedha za
kigeni kuwalipa wafanyikazi hao wa kigeni.
Lakini msemaji wa Dangote Group Tony Chiejina aliambia BBC kwamba ufutaji huo hauna uhusiano na mfumuko.
Kampuni hiyo inasema kuwa ilikuwa inaimarisha biashara zake na kwamba kazi zengine zimechukuliwa na kampuni tanzu.
Kampuni ya Dangote Group ni miongoni mwa kampuni zilizo na wafanyikazi wengi katika sekta hiyo.
Miezi
miwili iliopita ,kitengo cha habari cha Bloomberg kiliripoti kwamba
bwana Dangote alipoteza dola bilioni 5.4 mwaka huu kutokana na kuanguka
kwa thamani ya sarafu ya Nigeria ,Naira.
Post a Comment