Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mfuko wake maalum wa kusaidia
jamii wa Airtel FURSA Tunakuwezesha leo imekabidhi hundi ya shilingi
milioni 20 kwa Mbunge wa Nzega ikiwa ni harakari za kukamilisha dhamira
yake ya kushirikiana na jamii katika kuinua vijana sehemu mbalimbali
hapa nchini.
Akikabidhi hundi hiyo Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sunil Colasa alisema “Airtel imejipanga kwa kuhakikisha vijana wanaendelea kunufaika na mradi wa Airtel FURSA kwa kuwapatia misaada ya kukamilisha mipango yao waliyoipanga kwa kupunguza changamoto walizonazo ikiwemo ya ukosefu wa ajira na mtaji ili watimize malengo yao katika biashara”
“Tunaamini kupitia ushirika wetu na Mbuge Nzega Mh, Hussen Bashe mfuko wa Nzega Trust Fund utasaidia wananchi ndani ya vijiji 21 katika jimbo hilo ambapo malengo yetu ni kufanya mradi huu kuwa endelevu hata kwa majimbo mengine nchini” alisema Bw, Colasa
kwa upande wake Mbunge wa Nzega Mjini Mh, Hussen Bashe aliishukuru Airtel nakuahidi kusimamia mradi huo wa ukopeshaji kwa ajili ya kuweza kuinua vipato vya wananchi wa Nzega kama ilivyokusudiwa
“Nitoa wito kwa wananchi wote wenye malengo ya kujiendeleza kujitoza na kujisajili katia Mfuko wetu wa Nzega Trust Fund niliouanzisha kwaajili ya kuhakikisha tunaungana na wadau wenye nia ya kusaidia jamii kama Airtel FURSA ili kupunguza changamoto za maendeleo kwa wananchni hasa kwa wanaokosa mitaji ya kuendesha Miradi yao mbalimbali”
“Airtel tayari wamezikabidhi pesa hizi kwangu ambazo tutazikopesha kwenu kwa Riba ya 1.5% pale unaporejesha na faida inayopatikana bado itaendelea kuwasaidia vijana wengine watakaotaka kukopa” Alieleza Mh Bashe
Mradi wa Airtel Fursa umeanzishwa Mei mwaka uliopita na tayari umewafikia vijana zaidi ya Elfu tano kutoka katika mikoa kumi nchini ikiwa ni pamoja na vijana zaidi ya 100 waliowezeshwa kwa kupewa mitaji na vitendea kazi mbalimbali
Programu hii kati ya Airtel na Nzega Trust Fund chini ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe, itawawezesha zaidi ya wajasiriamali 350 kunufaika na mikopo kupitia huduma ya Airtel Money. Mikopo hii itatolewa kwa kikundi kilichoundwa na vijana watano ambao watapewa mtaji kati ya shilingi Shs.100,000 hadi 1,000,000 kulingana na mahitaji yao. Sambamba na mikopo ya WanaNzengo Airtel FURSA vikundi vya wajasirilamali vitaendelea kupewa mafunzo ya ujasiriamali ikiwa ni pamoja na namna ya kuendesha vikundi pamoja na jinsi ya kutafuta soko.

Mbunge
wa jimbo la Nzega Mjini Mhe, Hussein Bashe (kushoto) akiongea na
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso (kulia) wakati
alipotembelea ofisi za Airtel juu ya program ya WanaNzengo Airtel FURSA
inayowawezesha vijana wajasiriamali waishio katika kata 10 zilizoko
ndani ya Jimbo la Nzega Mjini mkoani Tabora kupata mikopo yenye riba
nafuu itakayosaidia kutatua changamoto za ajira kwa vijana. Programu hii
inaendeshwa kwa ushirika kati ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa
Airtel FURSA “Tunakuwezesha” na asasi iliyoundwa kimikakati na Mbunge
huyo ya Nzega Urban Trust Fund ili kumaliza tatizo la umasikini wa
kipato katika jimbo la Nzega Mjini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto), akikabidhi hundi
ya kiasi cha shilingi Milioni 20, kwa Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini
Mhe, Hussein Bashe (kulia) Kwa ajili ya kuwezesha vijana wajasiriamali
waishio katika kata 10 zilizoko ndani ya Jimbo la Nzega Mjini mkoani
Tabora kupata mikopo yenye riba nafuu itakayosaidia kutatua changamoto
za ajira kwa vijana. Programu hii inaendeshwa kwa ushirika kati ya
Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” na
asasi iliyoundwa kimikakati na Mbunge huyo ya Nzega Urban Trust Fund ili
kumaliza tatizo la umasikini wa kipato katika jimbo la Nzega Mjini.
Post a Comment