Kikundi
cha Makerubi kutoka Manyara ambao walijiandikisha wakitokea Temeke
waliweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika shindano la
Gospel Star Search 2016 kwa kuweza kuimba kwa ustadi mkubwa. Shindano la
Nusu fainali lilifanyika katika viwanja vya Biafra - Kindononi jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA
WA KAJUNASON BLOG.



Umati
wa watu waliohudhuria shindano la Gospel Star Search lililofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini
Dar es Salaam.
Mshiriki
namba 4. Grace Madole akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search
lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra -
Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu hakuweza kupenya hatua ya
fainali.
Mshiriki
namba 5. Winnypraise William akiimba katika jukwaa la Gospel Star
Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya
Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu alipenya kuingia
hatua ya fainali.
Shindano
la Gospel Star Search lilikuwa ni vuta nikuvute pamoja na mshiriki
namba 6. Willansia Lema kuimba kwa hisia ila hakuweza kufanikiwa kuingia
hatua ya nusu fainali ambayo iliweza kuingiza washiriki wapatao 10 na
kufanya washirikiki watano (5) kuaga mashindano.
Mshiriki namba 10. Flora Kachema alifanikiwa kuingia fainali.
Majaji
wa shindano la Gospel Star Search (GSS) kutoka kulia ni Mchungaji Sam
Mwangati, Sarah Ndossi na Fred Msungu wakiwa wamenyanyuka kuonyesha
heshima ya pekee kwa mshiriki ambaye aliweza kuvuta hisia zao.
Mshiriki mdogo kuliko wote akiwa aliwavuta hisia majaji wakajikuta wanatoa heshima ya pekee kwa kusimama.
Wageni waliohudhuria shindano hilo wakifurahia kwa shangwe.

Nderemo na vifijo vilitawala.
Mshiriki huyo akiwa amewateka wageni waliohudhuria na kujikuta wakiimba kwa hisia.
Mshiriki
Sunday Lunkombe alifanya vyema kuliko wenzake na kufanikiwa kuongoza
hakua ya kuingia fainali kwa kujizolea alama nyingi.
Washiriki wakionyesha umahiri wa kuimba pamoja kabla ya kutangazwa kumi bora.

Meneja
Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana
waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano
mkali.
Kiongozi
wa Majaji, Mchungaji Sam Mwangati akisoma majina ya vijana walifanikiwa
kuingia hatua ya fainali ya shindano la Gospel Star Search 2016
lililofanyika katika uwanja wa Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita. Fainali za shindano hili zinatarajiwa
kufanyika jumapili ya Septemba 18, 2016 katika ukumbi wa Milado, Sinza
jijini Dar es Salam.
Post a Comment