0

 Mchezaji wa timu ya Kitogoro fc akimiliki mpira huku akiangalia agawe basi wapi katika mchezo wa jana septemba 2 na Kitogoro fc iliweza kuisambalatisha Mihumo city kichapo cha magoli 3 bila.


Mlinda mlango wa timu ya Kitogoro fc jana aliweza kulinda lango mpaka dakika 90 zinakamilika hakuweza kuruhusu kutishwa nyavu langoni kwake.


Ligi ya Alizeti cup Jana septemba 2 katika hatua ya robo fainali ilikamilishwa kwa mchezo mmoja kati ya timu ya Mihumo city dhidi ya Kitogoro fc mchezo uliotimua vumbi uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika mchezo huo timu ya Kitogoro iliweza kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3-0 magoli ya Kitogoro fc yalifungwa na Alois Luwongo dakika ya 34,Abdelehemani Ndwimbage dakika ya 59 na goli la tatu lilifungwa na Festo Mnai magoli hayo yalidumu mpaka dakika 90 na Kitogoro fc kuweza kuingia katika hatua ya nusu fainali.

Kapteni wa timu ya Mihumo fc,Shamte Mkara akizungumza na Mwanahabari wetu alisema mchezo huo mwamuzi hakuchezesha vizuri baada ya kapteni huyo kupewa kadi nyekundu huku akidai kosa ameonewa kwakuwa lilikuwa kosa lake kumwendea mwamuzi kumjusha mwenendo wa mchezo ulikuwa si mzuri uwanjani aliongeza kusema waamuzi wanatakiwa kuchezesha mpira kwa kufuata sheri ili kuweza kukuza vipaji kama hawatafuata sheria za soka vipaji vingi vitashuka. 

Nae kocha wa Kitogoro fc,Abdelehemani Ndwimbage alisema walitegemea kupata ushindi huu kwakuwa walijipanga vya kutosha pia aliongeza kujipa matumia kuisambalatisha timu ya Sido fc katika mchezo wa hatua ya nusu fainali mchezo utakaochezwa septemba 6 mwaka huu.

Ratiba ya hatua ya Nusu Fainali iliweza kutolewa na katibu wa chama cha mpira wa miguu Liwale (Lidifa) Bwana Nourdin Kazumari.

Tarehe 5/9/2016  HAWILI FC Vs NEW BOYS
Tarehe 6/9/2016  SIDO FC Vs KITOGORO FC

Mshindi wa tatu (3) atapatikana
Tarehe 8/9/2016  alitakayepoteza septemba 5 atacheza atakayepoteza septemba 6


FAINALI itakuwa Mshindi wa septemba 5 atacheza na mshindi wa septemba 6 


Post a Comment

 
Top