0
Tokeo la picha la SIMBA NA RUVU SHOOTING
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting katika muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Iliwachukua dakika saba Ruvu kupata bao lililowekwa kimiani na Abraham Mussa kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Vicent Angban baada ya mabeki wa Wekundu hao kuzembea kuondoa hatari.

Dakika tatu baadae Ibrahim Ajib aliisawazishia Simba kufuatia pasi safi iliyopigwa na winga Shiza Kichuya upande wa kushoto wa uwanja baada ya Maafande hao kushindwa kujipanga vizuri.

Mshambuliaji Laudit Mavugo alikosa nafasi za wazi dakika ya 19 na 23 baada ya Ajib kufanya kazi ya ziada kuichambua safu ya ulinzi lakini Mrundi huyo alikosa umakini.

Mavugo aliipatia Simba bao la pili dakika ya 48 baada ya kupokea pasi nzuri ya Ajib ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Ruvu.

Mwamuzi Ngole Mwangole kutoka mkoani Mbeya alimuonesha kadi nyekundu kiungo Jabir Aziz baada ya kumfanyia madhambi Muzamir Yassin.

Simba iliwatoa Mavugo, Saidi  Ndemla na Kichuya nafasi zao zikachuliwa na Fredrick Blagnon, Muzamir pamoja na Jamal Mnyate. Kwa upande wa Ruvu waliwapumzisha Frank Msese, Abraham Mussa na Claide Wigenge na kuwaingiza Baraka Mtui,Issa Kanduru na Renatus Kisase.

Huko mkoani Mtwara, Yanga imeshindwa kufurukuta baada ya kutoka suluhu na Ndanda katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nangwanda Sijaona.

Post a Comment

 
Top