Wanawake watano
waliovalia mabuibui na walioaminika kuvaa mikanda ya kujilipua walivamia
kituo kimoja cha polisi mjini Mombasa katika shambulio la kigaidi.
Maafisa
wa polisi nchini Mombasa wanasema kuwa walitibua jaribio hilo na
kufanikiwa kuwaua wanawake watatu huku wawili wakikamatwa.Polisi wanasema kuwa washukiwa hao waliwasili katika kituo cha polisi cha Central ili kuripoti kuhusu simu ya rununu ilioibiwa.
Na wakati malalamishi yao yalipokuwa yakichukuliwa mmoja wao alichukua kisu na kuwadungu maafisa wawili wa polisi ,huku mwengine akiwarushia polisi waliokuwa wakichukua malamishi hayo bomu la petroli.
Maafisa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini huku kituo hicho cha polisi kikilindwa ili kuhakikisha kuwa hakuna tishio jingine.
Post a Comment