Leo September 19 2016 Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi
wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali kama ifuatavyo;
Kwanza, Rais Magufuli amemteua Prof. Jacob Philip Mtabaji kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuanzia tarehe 15 Septemba, 2016.
Prof. Jacob Philip Mtabaji anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Awadhi Mawenya ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa baada ya Kamisheni ya TCU kuvunjwa.
Pili, Rais Magufuli amemteua Prof. Mathew L. Luhanga
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe (MU) kuanzia
tarehe 29 Agosti, 2016. Prof. Mathew L. Luhanga anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Prof. Daniel Mkude ambaye amemaliza muda wake.
Tatu, Rais Magufuli amemteua Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kuanzia
tarehe 29 Agosti, 2016. Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake.
Nne,
Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudensia M. Kabaka kuwa Mwenyekiti wa
Baraza la Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016. Gaudensia M. Kabaka
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Augustine Mahiga ambaye kwa
sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Tano,
Rais Magufuli amemteua Mariam Mwafisi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia 05
Septemba, 2016. Mariam Mwafisi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Deogratias Ntukamazina ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua
Bw. Hetson Msalale Kipsi kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya
Kariakoo kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.
Post a Comment