0


Ni aibu ya aina yake katika soka la bongo. Pale mwamuzi wa akiba wa mchezo kati ya Toto African dhidi ya Mbeya City Joseph Masija alipoibiwa simu mbili za mkononi zenye thamani ya shilingi 500,000 na fedha taslim 140,000. 

Vitu hivyo viliibwa kwenye vyumba vya waamuzi hapo CCM Kirumba. Ni jambo la kuaibisha kama nini? Swali linalokuja kichwani kwangu ni hili: 

Uongozi wa uwanja huo umeshindwa kuweka ulinzi wa kutosha kwenye vyumba vilivyopo hapo uwanjani?? Swala la usalama wa watu na mali yao ni jambo ambalo ni lazima lipewe kipaumbele. Ina maana hata usalama wa waamuzi wenyewe uko mashakani. 

Kama anaweza kuingia vyumba vya waamuzi bila mtu yoyote kumuona na kuiba vitu, Je hawezi akamuwekea mwamuzi vitu vyenye kuhatarisha uhai. Tafadhali hili jambo liangaliwe kwa jicho la kipekee ili lisijirudie tena

chanzo: michezoforums

Post a Comment

 
Top