0


 Kampuni ya simu ya Apple imezindua rasmi simu yao mpya siku ya usiku wa Jumatano ya Septemba, 7 jijini San Fransisco iliyokua ikisubiriwa na watu wengi duniani, kutokana na ushindani mkubwa iliokua nayo na makampuni mengine ya simu.

Iphone 7 ambayo imefikia kiwango kikubwa cha kiteknolojia ikiwa imekuja na vitu mbalimbali ikiwemo mfumo mpya na wa kisasa wa kamera, uweza wa kuitumia ndani ya maji, rangi mpya aina ya jet black.

Mambo 7 mapya ndani ya simu mpya ya iphone 7.

1. Umbo la aina mbili iphone 7 yenye 4.7-inch na iphone 7 plus yenye 5.5-inch zote zikiwa na muonekano mpywa wa “high gloss jet black” zikiwa zimetengenezwa na mfumo wa 7000 series aluminum.

2. Kiwango cha dhahabu nyeusi (The gold standard of black)

3. Uwezo wa kuzuia maji (Built to be water resistant)

4. Mfumo mpywa wa home button ambayo kwa sasa imekuja na kifaa kinachoitwa (taptic engine)

5. Kamera mpya na ya kisasa yenye uwezo wa kuweka sawa picha (optical image stabilization, an ƒ/1.8 aperture, and a six-element lens)

6. Mfumo mpya wa flash uitwao (Quad-LED True Tone flash)

7. Kamera ya mbele maarufu kama (facing camera) yenye uwezo wa 7mp
 Apple watch mpya ya I Phone 7

Sambamba na hayo, kampuni hiyo imekuja na saa mpya aina ya apple watch series 2, ikiwa na mfumo wake wa GPS unao kuwezesha kuacha simu yako na kuendelea kupata viwango vyote vya umbali wakati wa mazoezi, kutembea au hata katika safari za hapa na pale.

Yajue hapa mambo mapya katika apple watch series 2.

1. GPS ya kujitegemea

2. Uwezo wa kutoingia maji mpka kufikia umbali wa mita 50

3. Kioo angavu

4. Uwezo wa kupima mapigo ya moyo

5. Program za mazoezi zote ndani yake.
 Bei za simu hizi za I Phone 7 inaanzia Dola 649 kwa I Phone 7 na Dola 749 kwa I Phone 7 Plus.
AirPod mpya za I Phone 7 ambazo ni wireless

Post a Comment

 
Top