0

Mchezo kati ya timu ya Super earlge (waliovalia brown) dhidi ya Likongowele fc
Ligi ya Nangando under 17 imeanza kutimua vumbi septemba 17 katika uwanja wa shule ya msingi Muungano wilayani Liwale huku lengo kuu la ligi hiyo ni kuibua vipaji wilayani Liwale.

Ligi hii inashirisha  jumla ya timu 7 zilizothibisha kushiriki ikiwa ni Everton fc,Likongowele fc,kigamboni fc,super earlge fc,Nangando city,Red star na the heroers.

Mchezo wa ufunguzi kulikuwa na mchezo kati ya timu ya Nangando fc 2-3 Likongowele fc, septemba 18 kulikuwa na mchezo kati ya Kigamboni fc 3-3 Evertoni fc, septemba 19 The Herroers 3-2 Super earlge, septemba 20 Everton 4-0 Red star, septemba 21 Nangando city 2-3 Super Earlge, septemba 22 The Heroes 3-2 Likongowele fc, septemba 24 Nangando city 0-0 The Heroers.

Leo septemba 25 kulikuwa na mchezo kati ya Super earlge 2-1 Likongowele fc  mchezo uliopigwa uwanja wa shule ya msingi muungano wilayani Liwale.

 Magoli ya Super earlge katika kipindi cha kwanza na goli la pili likifungwa kipindi cha pili huku goli la kufutia machozi la Likongowele fc ilifungwa kipindi cha pili kwa mkwaju wa penaiti.

Post a Comment

 
Top