Diwani wa viti maalum CHADEMA Sara Mwajeka na
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakionyesha mfano wa sare za wanafunzi walizotoa msaada
Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakiwa tayari kukabidhi sare kwa wanafunzi
Hawa ni baadhi ya wanafunzi
mia mbili (200) wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa
kusaidiwa msaada wa pesa kwa ajili ya kununulia sabuni,nauli kila wiki
na sare za shule ya msingi.
NA FREDY MGUNDA,Iringa
ZAIDI
ya wanafunzi mia mbili (200) wanaoishi katika mazingira magumu
wanatarajiwa kusaidiwa msaada wa pesa kwa ajili ya kununulia sabuni na
nauli kila wiki na wanawake walionda timu maalum ya kutoa msaada kutoka
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Msaada
huo unatarajiwa kutolewa kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira
magumu kutoka kata nne zilizoko manispaa ya Iringa ambazo ni Miyomboni,
Igumbilo, Kitanzani na Ruaha na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 3.5
Akizungumza
wakati wa kuwakabidhi msaada wa sare za shule,viatu na soksi wanafunzi
hao, katika hafla fupi ya iliyofanyika katika shule ya msingi ya
Igumbulo, Diwani wa viti maalum CHADEMA Sara Mwajeka alisema kuwa
wameamua kuwasaidia wanafunzi hao kwa lengo la kuwapatia elimu bora japo
kuwa misaada hiyo haiwezi kumaliza shida zao.
Mwajeka
aliongeza kuwa wanafunzi wenye mazingira magumu wanatakiwa kusoma ili
taifa lipate wasomi wengi wenye tija ya kuisaidai nchi yao kuendelea
kiuchumi.
“Mimi
kama mama napata uchungu kuona wanafunzi wenye mazingira magumu
wanasoma kwa taabu huku wana uwezo mkubwa darasani,hivyo tunajitaidi na
kujikuna pale tunapoweza kuwasaidia wanafunzi nawaomba watu wenye uwezo
kuwasaidia wanafunzi wote wenye mazingira magumu” alisema Mwajeka.
Kwa
upande wake Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata aliwapongeza
timu ya wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) manispaa
ya Iringa kwa kutoa msaada huo ambao ni mkubwa kwa maisha ya wanafunzi
wanaoishi kwenye mazingira magumu.
“Tanzania
yetu kuna matajiri wengi sana lakini wanashindwa kuwasaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu lakini wakimama hawa wamejitoa kwa
kile walicho nacho kuwasaidia wanafunzi hao hivyo nami naunga mkono
kuendelea kuchangia watoto hawa” alisema Lyata
Aidha
Lyata aliwataka viongozi wa nchi kuwaangalia wanafunzi wanaoishi katika
mazingira magumu ili kufuata na kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo
kwani alikuwa anapenda sana elimu ili wananchi waweze kuongeza ufahamu
na kujua mbinu za kujitegemea na sio kuomba omba kila siku.
“Jamani
kusaidia wanafunzi wenye mazingira magumu hawana idikadi ya vyama,dini
wala makabila tunatakiwa kuwasaidia kutokana na uwezo wetu wa kifedha,mm
nimekuwa mwalimu kwa muda mrefu na nayajua matatizo ya wanafunzi wenye
mazingira wanavyosoma kwa taabu ni aibu kwa taifa kama Tanzania kuwa
wanafunzi wanaoteseka kama hawa” alisema Lyata.
Naye
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga aliwashukuru
timu ya wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Naibu
Meya, Joseph Lyata kuwa kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kwani
wamewapunguzia na kuwaondolea aibu iliyokuwa inawakumba kutokana na
umasikini wao.
“Wanafunzi
hawa walikuwa wanavaa sare ambazo zilikuwa zimechanika na ilikuwa aibu
kwa wanafunzi wengine lakini kwa msaada huu mmefanya wajisikie nao ni
matajiri na najua sasa watasoma kwa bidii bila kujiangalia wamekaaje
hongereni sana na karibuni tena kuendelea kuwasaidia wanafunzi hawa”
alisema Asenga.
Misaada
hiyo imetolewa na timu ya wanawake wa chama cha demokrasia na
maendeleo(CHADEMA) manispaa ya Iringa kwa lengo la kuwasaidia watoto
wenye mazingira magumu wasome wakiwa na furaha kwa kuwa nao ni binadamu
kama binadamu wengine.
Post a Comment