0

  
ajali songea 
Taarifa tulizozipata hivi punde jana usiku Jumatatu,Septemba 19,2016 ni kwamba Basi la New Force kutoka Dar es salaam kwenda Songea limepata ajali kwa kupinduka maeneo ya Kifanya kilomita kadhaa kutoka mkoani Njombe.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja usiku wa Septemba 19,2016 ambapo inaelezwa kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya Madaba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ACP Prudenciana Protas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo,yuko eneo la tukio na ameahidi kutoa taarifa rasmi hapo baadaye.

Tutawaletea taarifa kamili

Post a Comment

 
Top