Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia tiketi ya CCM Hussein Bashe
amesema Rais Dkt. John Magufuli siyo 'dikteta' kama baadhi ya watu
wanavyosema bali ni kiongozi mkali anayeshughulikia mambo ambayo
yalikuwa yamezoeleka nchini.
“Rais Dkt. John Magufuli siyo
'dikteta' kama maana halisi ya dikteta ilivyo , ila ni kiongozi ambaye
ni mkali ambaye anapingana na mambo ya kufanya mambo kwa mazoeza
'Business as usual' waliokuwa wamezoea kupiga dili bandarini kwa siku
mtu alikuwa anapata laki moja au mbili sasa hiyo imekoma” Amesema Bashe.
Aidha
kuhusu baadhi ya wananchi kulalamika kwamba pesa hazionekani mtaani,
Mbunge Bashe amesema kipindi alipoingia katika uongozi Rais Benjamin
Mkapa wananchi walilalamika kwamba pesa zimepotea ila baada ya muda
uchumi ukaimarika hivyo kwa sasa wananchi waipe muda serikali ya Rais
Dkt John Magufuli.
Kuhusu jitihada za kuleta maendeleo Jimboni
kake, Bashe ameeleza namna aambavyo ameanza kusaidia vijana ambapo
baadhi ya vijana wanaofanya kazi ya kushona wamepelekwa Moshi kujifunza
namna ya kutengeneza viatu vya ngozi kwa kuwa jimboni humo anatarajia
kujenga kiwanda kidogo cha ngozi.
Pamoja na hayo Bashe amewataka
wawekezaji ambao wanataka kwenda kuwekeza katika jimbo lake kwenda kwa
kuwa watapatiwa ushirikiano wa kutosha na eneo la ardhi tayari lipo.
Post a Comment