Idadi
ya watu waliofariki katika ajali ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji
haramu wanaokadiriwa kufikia mia sita, iliyozama nje kidogo ya pwani ya
Misri imeongezeka na kufikia 42.
Mamlaka nchini humo zinasema mpaka sasa watu wengine laki moja na hamsini wameokolewa.
Mmoja
wa ndugu wa wahamiaji hao waliokuwa ndani ya boti Hassan Suleiman
Daoud, amezitupia lawama, mamlaka nchini Misri kwamba zilikuwa
zikishughulikia tatizo hilo taraatibu.
''...Tuliziambia
mamlaka husika tangu majira ya saa kumi na moja na nusu kwamba boti
inazama, lakini walikuwa wakisema hakuna boto ya uokoaji, na hakuna
aliyekuwa akishughulikia...'' alisema Hassan.
Amefahamisha
pia kwamba boti zao za uvuvi ndizo zilikuwa zikifanya kazi ya kuitafuta
boti hiyo na kuokota maiti baharini na watoto pia kutoka ndani ya maji.
Amefahamisha
pia kwamba wafanyabiashara haramu ya wahamiaji, wanatambuliwa na polisi
katika maeneo haya pia amelaumu kuwa huchukua malipo ya mwezi kutoka
kwao.
Katika
kipindi cha mwaka huu pekee, wahamiaji wapatao laki tatu wamekatisha
bahari ya Mediteranea na kuingia barani Ulaya, lakini njia yao kubwa ni
ile ya kutokea Libya.
|
Post a Comment