0


August 28 2016 Ligi Kuu soka Tanzania bara leo imeendelea kutimua vumbi kama kawaida kwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya African Lyon katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza kwa Yanga katika msimu wa 2016/2017 wakati African Lyon huu ni mchezo wa pili toka wapande Ligi Kuu msimu huu baada ya kushuka daraja misimu kadhaa nyuma, katika mchezo huo Yanga ambao ni Mabingwa watetezi wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0.

Magoli ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 19 na Simon Msuva dakika ya 60 kipindi cha pili, baada ya hapo kocha wa Yanga Hans van Pluijm alifanya mabadiliko ya kumtoa Simon Msuva na kumuingiza Juma Mahadhi aliyeenda kupachika goli la tatu dakika za nyongeza, hilo linakuwa goli la kwanza la Mahadhi toka ajiunge na Yanga.

Matokeo ya mechi nyingine za VPL zilizochezwa leo August 28 2016
  • Toto Africans 0-1 Mbeya City

Post a Comment

 
Top