0

 Mchezaji wa timu ya Wood pecker mwenye jezi nyeupe akikimbiza mpira



Michuano ya Ligi ya alizeti cup leo agosti 11 iliendelea kutimua vumbi tena kwa mchezo mmoja kati ya Black star dhidi ya Wood pecker mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Timu ya Wood pecker ilikuwa timu ya kwanza kufunga goli katika dakika ya 27 goli lililofungwa na Ashirafu Yusufu na timu ya Black star waliweza kusawazisha goli hilo  lililofungwa na Chalesi Chonde dakika ya 38 na kufanya mapumziko ikiwa sare ya goli 1 kwa 1.

Katika kipindi cha pili timu ya wood pecker iliweza kubadili mchezo na kucheza mchezo wa kasi huku walikuwa wanashambulia sana lango la Black star na waliweza kutumia nafasi vema na  Ashirafu Yusufu aliweza kufumania nyavu za Black star  kwa kupachika  magoli 2 aliofunga dakika ya 51 na 57.

Dakika ya 61 na 80 Shedraki john mchezaji wa timu ya Black star aliweza kusawazisha magoli mawili yaliyofanya kuweza kumaliza dakika 90 matokeo kuwa sare Black star 3-3 Wood pecker na mwamuzi wa mchezo akaamua kupigwa mikwaju ya penaiti.

Hatua ya mikwaju ya penaiti  timu ya Black stariliweza kuvumalia nyavu mara 2 na kukosa penaiti 3 huku timu ya Wood pecker iliweza kufumania nyavu kwa mikwaju yote 5 na kuweza kushinda jumla ya magoli 8 na Black star ikiwa imefunga magoli 5

Wood pecker wameweza kusonga mbele kwenye ligi hii na Black star wameondolewa kwenye mashindano haya.

Kocha wa timu ya Black star Mpalama Mshamu alisema amekubali matokeo lakini hakulizika katika hatua ya upigaji wa penaiti kwa kusema mwamuzi wa mchezo wachezaji wake alikuwa  hawajawatendea haki alikuwa anawashughulisha sana na kila wanapopiga mpira mwamuzi alikuwa anaenda sehemu ya mpira kuelekeza hali iliyopelekea wachezaji wa Black star kukosa kujiamini na kocha wa Wood pecker Emmanuel Silayo alisema mchezo ulikuwa mzuri japo kulikuwa na dosali ndondogo.

Agosti 12 kutakuwa na mchezo ungine utakaowakutanisha timu ya New generation dhidi ya Nangando city mchezo utaopigwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni.


 KUANGALIA MATOKEO YA LIGI YA ALIZETI CUP YA MCHEZO WA JANA BOFYA >>HAPA

KUNGALIA RATIBA YA LIGI YA ALIZETI CUP BOFYA >>HAPA

Post a Comment

 
Top