0

 Ni miongoni mwa faulo walizoweza kupata timu ya Vijuso fc lakini hawekuweza kutumia vema


 Mchezaji mwenye jezi ya punda wa timu ya Vijuso fc akijaribu kumtoroka mchezaji wa timu ya Mikunya fc
 Mpira uliopigwa kuelekea lango la timu ya Vijuso fc
Ligi ya Alizeti cup 2016 imeanza rasmi leo agosti 10 kutimua vumbi katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,timu zilizofungua dimba ni MIKUNYA FC  na VIJUSO FC na katika ligi hii kuna jumla ya timu 13 kutoka kanda ya Liwale zinazoshiriki mashindano haya  ikiwa dhumuni kuu ni uhamasishaji wa wakulima kulima zao la Alizeti hapa wilayani.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Mikunya fc ilikuwa ya kwanza kupata goli mwanzo mwa dakika ya 9 goli lililofungwa na Mustafa Dili lakini goli hilo halikudumu huku timu ya Vijuso fc walisawazisha goli hilo dakika ya 15 kwa njia ya mkwaju wa penaiti uliopigwa na Yuba Mmocha.

Dakika ya 33 Vijuso fc walipata goli la pili lilofungwa na Shafii Twalibu na Mikunya fc waliweza kusawazisha katika dakika ya 43 kupitia kwa mchezaji wao Hamisi Malobe huku dakika 45 zikimalizika timu zote zilienda mapunziko zikiwa sare ya magoli mawili kwa mawili. 

Katika kipindi cha pili Mikunya fc namo dakika ya 46 na 49 Mustafa Dili aliweza kuifungia timu yake na vijuso fc waliweza kufunga goli la 3 dakika ya 54 kupitia kwa mchezaji wao Yuba Mmocha.

Mpaka dakika 90 zinakamiliza na mwamuzi kumaliza mpira matokeo yalikuwa Mikunya fc 4-3 Vijuso fc na mwa mujibu wa tarabu ya mashindano haya ni mtoani hivyo timu ya Mikunya fc imeweza kusonga mbele na timu ya Vijuso fc imetoka kwenye mashindano.

Katika mchezo wa leo mashabiki wengi wa hapa Liwale mjini walikuwa wanaishangilia sana timu ya kutoka nje ya Liwale mjini ambayo ni timu ya Mikunya fc kwa mchezo waliouonsha leo uwanjani.

Kocha wa timu Mikunya fc Ali Mkulage alisema mchezo ulikuwa mzuri licha ya kushindi lakini maandalizi ya wachezaji hayakuwa mazuri huku akijihakishia mchezo ujao kufanya vizuri zaidi kwa upande wa Kocha wa Vijuso fc Haji Mtutuma alisema walipata nafasi nyingi kuweza kufunga  lakini hawakuweza kutumia nafasi hizo vizuri huku wapinzani wao waliweza kutumia nafasi walizopata na kuzitumia vizuri pia alikubali matokeo ya mchezo kwa kufungwa magoli 4 kwa 3 na kuondolewa kwenye mashindano.

Kesho agosti 11 kutakuwa na mchezo ungine utakaowakutanisha timu ya Black star dhidi ya Wood pecker mchezo utaopigwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni.


Post a Comment

 
Top