Winga wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu ya Leicester City kuhusishwa kuondoka King Power msimu huu inawezekana zikawa zimemalizika, Riyad Mahrez anaripotiwa na The Guardian kuwa amekiri kuwa Leicester City hawawezi kumuachia aondoke msimu huu.
Stori kutoka The Guardian pia zinaeleza kuwa Leicester City wameanza kumsahawishi Mahrez aongeze mkataba mpya, licha ya kuwa mkataba wake wa sasa unamalizika 2019 lakini maboss wa Leicester wanaripotiwa kuanza mazungumzo na staa huyo.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Riyad Mahrez kwa sasa anawindwa na vilabu vya Arsenal na Chelsea na kwa kiasi kikubwa Arsenal wamekuwa wakiandikwa zaidi kukaribia kunasa saini ya staa huyo, August 10 Arsenal wanaripotiwa kuwa walituma ofa ya pound milioni 35 lakini zilikataliwa na Leicester City.
Post a Comment