Waumimi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki,
Kanisa Kuu la Mtwara wameingia katika ibada na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali
wa kumpinga Askofu Mkuu wa dayosisi hiyo, Lucas Mbedule kwa tuhuma za kukiuka katiba,
unyanyasaji wa watumishi na ubadhilifu wa fedha za ushirika na dayosisi.
Hata hivyo, Askofu Mbedule amesema asingependa kuyazungumzia suala hilo kwa sababu
walikaa kikao.
Umoja wa wazee ulitoa tamko ndani ya kanisa hilo kutokana na tuhuma zinazomkabili askofu
huyo na kumtaka asijihusishe na mambo yanayohusu usharika na dayosisi, ili kupisha
uchunguzi na kumwomba Mkuu wa KKKT, Dk Fredrick Shoo kuunda tume kuchunguza
tuhuma hizo.
Akisoma tamko la wazee wa kanisa hilo, Amon Mkocha amesema wanapinga uamuzi
uliofanywa na kikao cha halmashauri kuu kilichofanyika mwezi huu
Post a Comment