0


 Mchimbaji wa kisima aliyefahamika kwa majina ya Waziri Omary (25) mkazi wa Ngaramtoni amefariki dunia kisimani wakati akichimba kisimani.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amekiri kutokea kwa tukio hilo marehemu alikutwa amefariki kisimani baada ya  kuwasha moto wa mkaa ili kulainisha mwamba ili aweze kupata maji kwenye kisima  chenye urefu wa futi 60, alikutwa saa 5 juzi akiwa ameshapoteza maisha.

"Kilichotokea ni kwamba huenda wakati amewasha jiko, Carbonmonoxide ilizidi huku hewa ya Oxygen ilikuwa ndogo kiafya lazima angedhurika. Mwili wa marehemu haujakutwa na jeraha  lolote, tunaendelea na uchunguzi kubaini zaidi , "alisema Kamanda. Pia amewatahadharisha watu kuhakikisha watu nawapotumia majiko ya mkaa ndani kuhakikisha kuna hewa ya kutosha..

Post a Comment

 
Top