Wananchi wakimsikiliza diwani wa Kata ya Mlowo Sebastian Kilindu akiwasihi kuwa na utulivu
Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe akiongea na wananchi wa Mlowo ili kusuluhisha mgogoro.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa dada wa marehemu eneo la Mlowo Mbozi Mkoani Songwe.
Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe akiongea na wananchi wa Mlowo ili kusuluhisha mgogoro.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa dada wa marehemu eneo la Mlowo Mbozi Mkoani Songwe.
Hali
ya uvunjifu wa amani umejitokeza mji mdogo wa Mlowo Wilaya ya Mbozi
Mkoani Songwe baada ya wananchi kuchoma moto barabarani kwa magurudumu
ya magari barabara Kuu ya TANZAM Mbeya/Tunduma.
Tukio hilo limetokea leo Agosti 28,2016 majira
ya mchana baada ya wananchi wa Mlowo kudai kuwa mkazi mmoja
aliyefahamika kwa jina la Stanslaus Kalinga (42)kupigwa na askari baada
kukamatwa kwa kosa la uzembe na uzururaji.
Marehemu amefia hospitali ya Wilaya ya
Mbozi akipatiwa matibabu.Diwani wa Kata ya Mlowo Sebastian Kilindu
amekiri kutokea kwa tukio hilo na baadaye alikwenda Polisi ili kupata
ukweli wa tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Mathias
Nyange amesema kuwa Jeshi la Polisi lilimkamata marehemu na hakupigwa na
Polisi kama inavyodaiwa kwani taarifa kamili juu ya kifo hicho ataitoa
baada ya uchunguzi wa Daktari.
Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa
Mlowo walibeba chakula kutoka msibani na kunipeleka kituo cha Polisi
Mlowo kwa kile walichodai kifo cha marehemu kimesababishwa na Askari
hivyo nao washiriki kula.
Hali hiyo ilisababisha polisi kutumia mabovu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao .
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mlowo
alimuomba Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe kufanya suluhu na wananchi hao
kwa kuwa Askari hawana kambi wanaishi nao mitaani hivyo mgogoro huo
utatuliwe kwa amani .
Hata hivyo bado hali imekuwa tete kutokana na wananchi kughadhabika.
Chanzo-Mbeya yetu blog
Post a Comment