0

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara katika jiji la Dar es salaam kuboresha taarifa za usajili wa namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ili kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa namba hiyo.

Uhakiki huo utaiwezesha mamlaka hiyo kuweza kujua idadi sahihi ya wafanyabiashara walipa kodi, kuondoa walipa kodi hewa ambao wamekuwa hawajihusishi na biashara kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo au kufungwa kwa makampuni yao.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Alphayo Kidata amesema mfumo huo utawawezesha wafanyabi

Kidata amesema kuwa mfumo wa sasa wa uhifadhi kumbukumbu za walipa kodi ulikuwa na kasoro nyingi hivyo mfumo mpya utaendana na ukuaji wa teknolojia na kukuza uchumi.

“Zoezi hili linamtaka kila mwenye namba ya utambulisho yani TIN kufika katika ofisi za TRA zilizopo karibu naye bila kuwakilishwa na mtu yeyote na zoezi litatumia dakika 10 kumalizika” amesema

Naye Elija Mwandubya ambaye ni kamisha wa mapato wa ndani wa mamlaka hiyo, amesema zoezi hilo litachukua siku 60 na kuanzia Dar es salaam na baadaye kuhamia mikoa mingine ndani ya nchi.
“TRA ina wafanyabiashara walipa kodi milioni mbili na laki moja hivyo uboreshwaji wa TIN utatupa uelewa wa idadi kamili ya walipa kodi” Amesema

Elija amesema kutakuwa na vituo maalum kwaajili ya uhakiki wa taarifa katika mikoa ya kikodi ambapo Kinondoni wafanyabiashara watatakiwa kutembelea ofisi za TRA zilizopo jengo la LAPF – Kijitonyama na Kibo Complex Tegeta.

Ilala wafanyabiashara watembelee ofisi ya TRA shauri moyo na 14 Rays Gerezani na Temeke wafike ofisi za uwanja wa Taifa.

Post a Comment

 
Top