0

Timu ya Yanga na Azam FC zinatarajiwa kukutana kesho Jumatano katika mechi ya Ngao ya Hisani ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17, tayari kila upande unaonekana kuwa tayari.

timu ya Yanga ambao upande wa uongozi kwa sasa hakujatulia kutokana na taarifa za mwenyekiti wao, Yusuf Manji kutaka kujiuzulu nafasi hiyo, kikosi chao kipo kwenye mazoezi katika Uwanja wa Gymkhan jijini Dar es Salaam wakati Azam FC wao wapo kwenye Uwanja wao wa Azam Complex nje kidogo ya Dar es Salaam.

 Timu hizo ambazo katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa na ushindani mkali zitakutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kutokana na Yanga kuwa bingwa wa Ligi kuu Bara wakati Azam ilishika nafasi ya pili katika Kombe la FA, hivyo kwa kuwa kanuni inataka bingwa wa FA na ligi kuu kukutana ilibidi Yanga icheze na Azam kwa kuwa Yanga pia ilichukua ubingwa wa FA.

Kila upande unaonekana kuwa fiti kwa mchezo huo japokuwa Yanga itakuwa na wachezaji kadhaa majeruhi ambao watakosekana katika mchezo huo baadhi yao ni Geofrey Mwashiuya, Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Post a Comment

 
Top