0

Wadau mbalimbali wa zao la Korosho wakipata picha mara baada ya kufanyika mkutano Bagamoyo mkoani Pwani.
 
Serikali imewaagiza wakuu wa mikoa 12 inayolima zao la Korosho nchini kuhakikisha msimu ujao wa mwaka 2016-2017 hakuna Korosho itakayouzwa nje ya mfumo wa ukusanyaji kodi , vinginevyo hatua staiki zitachukuliwa dhidi ya watakaozembea agizo hilo.

Agizo hilo limetolewa na waziri wa kilimo mifugo na uvuvi  Mh Charles Tizeba wakati akifungua mkutano mkuu wa wadau wa zao la Korosho unaofanyika Bagamoyo mkoani Pwani na kusisitiza serikali haitakubali kuona kila msimu wa Korosho inapoteza mapato, huku baadhi ya wakuu wa wilaya wakisema wamejiandaa vyema kupambana na utoroshaji wa mazao pasipo kulipiwa kodi.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge waliohudhuria mkutano huo mbunge wa jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota amekiri ukwepaji kodi katika zao la Korosho ni changamoto inayoitaji kufanyiwa kazi.

Mkutano huo wa siku mbili unaudhuriwa na wajumbe mia sita wakiwemo, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri na baadhi ya wakulima.

Post a Comment

 
Top