Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati
ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa
ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max
Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart, Mhandisi Juma Rajab,
akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo
na Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo,
walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba
kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.
Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.
Mkuu wa Oparesheni wa Chumba cha
kuangalia mienendo ya mabasi ya udart yakiwa barabarani, Mhandisi
Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo mbele ya wajumbe wa kamati
hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo unavyofanyakazi.
***
Kamati ya bunge ya tawala za mikoa na
serikali za mitaa leo asubuhi imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea
mradi wa Udart yenye lengo la kujua jinsi mradi huo unavyoendeshwa
pamoja na kujua changamoto zake ambapo wajumbe hao waliongozwa na
Mwenyekiti wao Jasson Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba vijijini.
Katika hatua nyingine ya ziara hiyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kuhakikisha anawaondoa wafanyabiashara katika
Miundombinu ya Kampuni ya Mabasi ya mwendo wa haraka (Udart)
Simbachawene alitoa agizo hilo wakati
akizungumza na uongozi wa Udart baada ya kufanyika majuisho ya ziara ya
kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kutembelea mradi
wa Udart Dar es Salaam leo.
"Namuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwaondoa mara moja wafanyabiashara katika miundombinu ya udart" alisema Simbachawene.
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa
alisema changamoto kubwa iliyopo ni elimu kwa wananchi kuhusu matumizi
ya miundombinu ya udart.
Alisema changamoto waliyonayo ni
wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya miundombinu ya
udart ambapo wamejipanga kuhahikisha kila mwananchi anaipata jambo
litakalosaidia kuitunza na kuendelea kupata huduma bora.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson
Rweikiza aliutaka uongozi wa udart kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma
bora za usafiri jijini Dar es Salaam ili kuwapunguzia adha ya usafiri
wananchi.
Kamati hiyo ilitembea mradi wa udart
katika vituo vikuu vya Kimara mwisho, Moroco makao makuu ya Udart
Jangwani, Gerezani na Kivukoni.
Post a Comment