Hakuna Jambazi yeyote aliyeuawa katika tukio hilo zaidi ya afisa huyo wa polisi.
Licha
ya viongozi hao kukataa kuzungumza, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili ambaye alikuwa bega kwa bega na
askari hao alisema kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wanaume 7 ambapo
walikutwa wanaume 3 na wanawake 3 ambapo mwanaume mmoja aliyetajwa
kumuua Afisa huyo wa Polisi alitoroka pamoja na silaha yake.
Mapaparazi
wetu baada ya kufika eneo hilo walitaka kuzungumzia na maofisa wa
polisi waliokuwa eneo hilo akiwemo, RPC wa Pwani, Bonaventura Mushongi,
Gilles na Kamishna Mwandamizi wa Jeshi hilo, Liberatus Sabas lakini wote
walisema hawawezi kuongea chochote mpaka wapate ruhusa kutoka ngazi za
juu kwa kuwa tukio hilo si la Kimkoa bali ni la Kitaifa.
Baada
ya jambazi huyo kumuua askari, jeshi la polisi liliongeza nguvu eneo
hilo na kupiga mabomu na risasi nyingi hewani zilisababisha taharuki
katika eneo hilo na kusababisha kila mmoja aseme lake.
Eneo
la Mtaa wa Vikindu Mashariki mkoani Pwani kwenye nyumba ya mtu mmoja
aliyetajwa kwa jina la Mzee Manitu paligeuka uwanja wa mapambano baada
ya polisi kuizingira nyumba hiyo na kupiga risasi nyingi hewani wakati
wakimtaka jambazi anayetuhumiwa kufanya mauaji ya katika tukio la kuuawa
askari polisi wanne waliokuwa wakibadilishana lindo kwenye Benki ya
CRDB Tawi la Mbande wialayani Temeke jijini Dar. Katika tukio hilo Afisa
wa Polisi mwenye cheo cha ASP Thomas Njuki wa Kikosi Maalum cha
Kupambana na Ujambazi ameuawa.
Eneo la Mtaa wa Vikindu Mashariki mkoani Pwani kwenye nyumba
ya mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Mzee Manitu paligeuka uwanja wa
mapambano baada ya polisi kuizingira nyumba hiyo na kupiga risasi nyingi
hewani wakati wakimtaka jambazi anayetuhumiwa kufanya mauaji ya katika
tukio la kuuawa askari polisi wanne waliokuwa wakibadilishana lindo
kwenye Benki ya CRDB Tawi la Mbande wialayani Temeke jijini Dar. Katika
tukio hilo Afisa wa Polisi mwenye cheo cha ASP Thomas Njuki wa Kikosi
Maalum cha Kupambana na Ujambazi ameuawa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikindu Mashariki, Mohammed Ismaili
Angalia picha
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/ ISSA MNALLY /GPL
Post a Comment