0
 
HISTORIA YA TIMU YA NEW GENERATION
Ligi ya Alizeti cup agosti 12 imeendelea kutimu vumbi kwa mchezo mmoja kati ya New generation dhidi ya Nangando city mchezo uliochezwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkaoni Lindi.
Timu ya new generation iliweza kupata goli la kuongoza mwanzoni mwa dakika ya 6 lililofungwa na Mawazo Kiwima na goli hilo kudumu mpaka mapumziko wa dakika 45.
Kipindi cha pili Timu ya Nangando city iliweza kupata nafasi nyingi za kushambulia lango la New generation lakini walishindwa kutumia nafasi hizo vema.
Katika dakika za lala salama Huseni Mchite waliifungia goli New generation dakika ya 81 na kuwafanya New generation kucheza kwa kulinda goli na kuwafanya kumaliza mpira mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa New generation 2-0 Nangando city. HABARI ZAIDI BOFYA >>HAPA
 
HISTORIA YA TIMU YA SIDO FC 
 
Agosti 14 katika ligi ya Alizeti cup katika kanda ya Liwale mjini kulikuwa na mchezo kati ya mabingwa wapya wa kombo la Ngo'ombe ililofanyika julai mwaka huu timu ya Sido fc dhidi ya Likongowele city mchezo ulipigwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Sido fc iliweza kuongoza kutikisa nyavu mara mbili katika lango la timu ya Likongowele city katika dakika za mwanzoni mwa mchezo na mwishoni magoli hayo yakifungwa na Haikosi Mpwate dakika ya 11 katika dakika ya 25 timu ya sido fc walipata penaiti lakini Haikosi Mpwate alikosa mkwaju wa penaiti na Yunus mbonde alipachika goli la pili katika dakika ya 44.

Katika dakika ya 64 timu ya Sido fc iliweza kuongeza goili la tatu lililowekwa nyavuni na Abuu kazumari na timu ya Likongowele city katika dakika ya lala salama iliweza kupata goli la kufutia machozi lililofungwa na Wamuzi Kaubaga namo dakika ya 81 na kufanya matokeo mpaka dakika 90 zinakamilika Sido fc 3-1 Likongowele city. HABARI ZAIDI BOFYA >>HAPA

Post a Comment

 
Top