Mchezaji wa timu ya New generation akiwa anakokota mpira
Mchezaji wa timu ya Nangando city akijaribu kupasia basi angalau akitafuta angalau goli la kufutia machozi lakini harakati za kufumania lango la New generation ziliota mbawa leo katika uwanja wa wilaya ya Liwale
Ligi ya Alizeti
cup leo agosti 12 imeendelea kutimu vumbi kwa mchezo mmoja kati ya New generation dhidi
ya Nangando city mchezo uliochezwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkaoni
Lindi.
Timu ya new
generation iliweza kupata goli la kuongoza mwanzoni mwa dakika ya 6
lililofungwa na Mawazo Kiwima na goli hilo kudumu mpaka mapumziko wa dakika 45.
Kipindi cha pili
Timu ya Nangando city iliweza kupata nafasi nyingi za kushambulia lango la New
generation lakini walishindwa kutumia nafasi hizo vema.
Katika dakika za
lala salama Huseni Mchite waliifungia goli New generation dakika ya 81 na
kuwafanya New generation kucheza kwa kulinda goli na kuwafanya kumaliza mpira mpaka
dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa New generation 2-0 Nangando city.
Kocha wa timu ya Nangando
city Ali Huki alisema mchezo ulikuwa mgumu katika kipindi cha kwanza timu yake
ilielemewa sana na nafasi walizopata hawakuweza kuzitumia vema katika kufumania
lango la New generation nae kocha wa New generation Bakari Mpalama alisema
licha ya kupata ushindi lakini baadhi ya wachezaji wake hawakuweza kucheza
kwakuwa ni majeruhi.
Agost 13 kutakuwa na mchezo kati ya timu ya
Abajalo Vs Polisi fc mchezo unaotarajiwa kuwa mkali utakaopigwa uwanja wa
wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni kwani katika mchezo huo timu ya Abajalo
fc ni kwa mara ya kwanza kushiriki ligi mwaka huu huku polisi fc waliwa
wakitaka kuonesha uwezo wao na kutaka ushindi.
Post a Comment