Serikali ya Australia kupitia Waziri Mkuu wa nchini hiyo, Malcolm Turnbull imesema kuwa mtandao wa ofisi ya takwimu ya nchi hiyo umeibiwa na kufungwa na waharifu wa mtandao ambao kwa mujibu wa taarifa walizozipata wapo nchini Marekani.
Turnbull alisema pamoja na taarifa za mitandao kuonyesha kuwa hackers hao wapo nchini Marekani lakini pia hawawezi kusema moja kwa moja watu hao wapo Marekani na hivyo bado wanafanya juhudi kuona kama wanaweza kurudisha mtandao huo.
“Sio rahisi kupata takwimu sahihi hasa kama unatumia mifumo tofauti na inayotumika katika sehemu nyingine … jambo hili limetokea kwa wakati ambao halikutarajiwa na linafanya watu kukosa takwimu,” alisema Turnbull.
Post a Comment