MABINGWA na wawakilishi pekee wa Tanzania Bara katika Caf
Confederation Cup 2016, timu ya Yanga SC kesho Jumamosi wataikabili MO
Bejaia ya Algeria katika mchezo wa kundi la kwanza. Yanga inaingia
kucheza game yake ya mwisho katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku
wakiwa na alama moja tu.
Bejaia tayari wana pointi tano sawa na Waghana, Medeama SC wakati Yanga ili ifuzu kwa nusu fainali watalazimika kushinda game zao zote mbili huku wakiomba TP Mazembe iifunge Medeama huku wao wenyewe wakifanya hivyo dhidi ya Waalgeria ambao waliwachapa 1-0 katika game ya kwanza mwezi June.
USHINDI
Ni kweli kitendo cha kupoteza game tatu na kutoa sare mara moja (Bejaia 1-0 Yanga, Yanga 0-1 Mazembe, Yanga 1-1 Medeama, Medeama 3-1 Yanga) kimewaweka njia panda mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Tanzania Bara.
Lakini kitendo cha kushinda game yoyote kati ya mbili zilizosalia (Yanga v Bejaia, Mazembe v Yanga) itakuwa ni mafanikio mengine makubwa kwao kwa maana hawajawahi kupata ushindi katika michezo takribani kumi ya hatua ya makundi.
Mwaka 1998, mabingwa hao mara 26 wa Bara walifuzu katika michuano ya ligi ya mabingwa lakini wakaambulia sare mbili tu na kupoteza game nyingine nne. Ushindi katika mchezo wowote kati ya miwili iliyosalia ni muhimu sana kwa Yanga kwa maana watakuwa wamepiga hatua fulani ya mafanikio.
Ni kweli nafasi ya Yanga ni finyu sana, lakini asilimia chache za matarajio zinaweza kubebwa na maajabu ya mchezo wa soka.
Medeama watakuwa wenyeji wa TP Mazembe ambao tayari wamefuzu kwa nusu fainali. Ikiwa mechi hiyo itamalizika kwa TP kushinda huku pia Yanga ikiwafunga Bejaia hapa Dar es Salaam itamaanisha kuwa, Bejaia na Medeama watabaki na alama zao tano tano na Yanga watakuwa na pointi nne.
Hivyo basi timu ya pili katika kundi itapatikana katika game za mwisho (Mazembe v Yanga, Bejaia v Medeama).
Yanga hawapaswi kukata tamaa kwa maana bado wapo katika mapambano. Wanaweza kushangaza ikiwa watafikisha alama saba ambazo ili kuzipata ni lazima wazifunge Bejaia siku ya kesho kisha TP katika game ya mwisho huko Lubumbashi.
Kocha Hans Van der Pluijm, benchi lake la ufundi na wachezaji naamini hawajawahi kupoteza matumaini ya kufuzu kwa nusu fainali, lakini mashabiki wa timu hiyo wengi wanaonekana kuvunjika mioyo yao hasa baada ya kupoteza 3-1 dhidi ya Medeama.
KUFUNGA MAGOLI
Yanga imefanikiwa kufunga magoli mawili tu katika mechi zote nne za michuano hiyo. Ni wastani wa chini sana kwa timu hiyo ambayo ina washambuliaji watatu wa kigeni.
Donald Ngoma alifunga katika sare ya 1-1 dhidi ya Medeama na mshambulizi huyo wa Zimbabwe amekuwa akiwekewa ulinzi mkali sana tangu alipoonesha kiwango cha juu katika Caf Champions league dhidi ya Al Ahly.
Amis Tambwe amekuwa na michuano migumu kimataifa kwa maana hajafanikiwa kufunga goli lolote katika game 11 za Caf. Mfungaji huyo bora wa ligi kuu Bara hakufunga goli hata moja katika game 6 za Champions league na hadi sasa Yanga ikiwa imekwishacheza game 6 katika Confederation Cup, raia huyo wa Burundi alikosa game dhidi ya Mazembe hajafunga pia.
Obrey Chirwa ndiye mchezaji aliyeingia katika soka la Tanzania kwa gharama kubwa zaidi (zaidi ya milion 200) yeye bado hajafunga katika game zake tatu alizoichezea Yanga. Washambuliaji hawa watatu wanapaswa kufunga sasa ili timu ipate matokeo kwa maana bila kufunga huwezi kushinda mechi.
KUTOENDEKEA KURUHUSU GOLI/MAGOLI
Hii ni nafasi ya mwisho kwa Yanga na dakika 90′ zijazo zinaweza kuwaondoa kabisa katika michuano ikiwa watapoteza mechi. Safu ya ulinzi ya timu hiyo imekuwa na matatizo makubwa hasa anapokosekana Mtogo, Vicent Bossou.
Katika game mbili dhidi ya Medeama wameruhusu magoli manne, na waliruhusu goli mojamoja katika mechi dhidi ya Bejaia na Mazembe. Timu nzima inapaswa kujilinda vizuri na kuhakikisha hawaruhusu kufungwa huku wakipambana kuhakikisha wanafunga.
PASI ZA MWISHO
Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Saimon Msuva/Deus Kaseke wanaweza kuanzishwa katika nafasi ya kiungo.
Wachezesha timu hao wameshindwa kutengeneza nafasi za kutosha na kupiga pasi za mwisho zenye mwelekeo. Ili washambuliaji wafunge magoli ni lazima viungo hawa watengeneze nafasi nyinyi na kupiga pasi za magoli.

Post a Comment