0

Kikosi cha Azam FC kipo kamili kujiandaa na mchezo wake wa kirafiki wa Kimataifa utakaopigwa leo usiku katika uwanja wao wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Azam FC ambao kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakijifua kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara, inatarajia usiku wa leo kucheza na URA FC klabu kutoka nchini Uganda mchezo ambao unatarajia kuwa ni mkali na kuvutia kwani timu hizo zimekuwa zikukutana katika michuano ya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1.00 usiku huku viingilio ikiwa ni Sh.1,000 kwa majukwaa ya kawaida huku jukwaa maalum la V.I.P likiwa ni Sh 3,000.

Post a Comment

 
Top