0

Timu ya Likongowele inahistoria ikifungwa huwa wanaanza rafu lakini leo ilikuwa tofauti sana na mechi za awali kwani leo waliweza kucheza mpira safi japo mashabiki wao wakiwaambia wacheze rafu


 Wachezaji wa timu ya Sido fc wakishangilia goli la tabu lilofungwa na Abuu kazumari namo dakika ya 64
Mchezaji  pia na kocha wa timu ya Likongowele city Wamuzi Kaubaga aliamua kuingia uwanjani ili kuweza kuisaidia timu yake na aliweza kuifungia goli la kufutia machozi katika dakika ya 81.

Leo ikiwa Agosti 14 katika ligi ya Alizeti cup katika kanda ya Liwale mjini kulikuwa na mchezo kati ya mabingwa wapya wa kombo la Ngo'ombe ililofanyika julai mwaka huu timu ya Sido fc dhidi ya Likongowele city mchezo ulipigwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika kipindi cha kwanza timu ya Sido fc iliweza kuongoza kutikisa nyavu mara mbili katika lango la timu ya Likongowele city katika dakika za mwanzoni mwa mchezo na mwishoni magoli hayo yakifungwa na Haikosi Mpwate dakika ya 11 katika dakika ya 25 timu ya sido fc walipata penaiti lakini Haikosi Mpwate alikosa mkwaju wa penaiti na Yunus mbonde alipachika goli la pili katika dakika ya 44.

Katika dakika ya 64 timu ya Sido fc iliweza kuongeza goili la tatu lililowekwa nyavuni na Abuu kazumari na timu ya Likongowele city katika dakika ya lala salama iliweza kupata goli la kufutia machozi lililofungwa na Wamuzi Kaubaga namo dakika ya 81 na kufanya matokeo mpaka dakika 90 zinakamilika Sido fc 3-1 Likongowele city.


Kesho agosti 15 kutakuwa na mchezo wa funga bimba kwa hatua hii ya mtoano ambapo kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya timu ya  Kigamboni fc vs Hawili fc Mchezo utakaochezwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10.

Timu zote za kesho agosti 15 ni za kiwango kwani ziliweza kukutana mara mmoja katika ligi ya Liwale super cup liliofanyika julai mwaka huu ambapo timu ya Hawili ilifungwa kwa njia ya mikwaju ya penaiti mara baada ya kucheza dakika 90 kukamilika ziliweza kufungana magoli 2 kwa 2 ndipo zikaenda kupigwa mkwaju ya penaiti.

Kanda ya Mihumo hapo agosti 13 iliweza kuanza mashinda haya ya Alizeti cup katika kanda hii kuna Jumla ya timu 3 zinazoshiriki ambazo ni timu ya  Turuka fc, mihumo city na super star.

Mchezo wa ufunguzi katika kanda ya Mihumo kulikuwa na mchezo kati ya timu ya Turuki fc dhidi ya Mihumo city katika mchezo huu timu ya Mihumo city iliweza kuipuluza Turuka fc goli 1 bila goli hilo lilifungwa na Amiri kikoweka katika kipindi cha pili dakika ya 75.

Pia nao hapo kesho Agosti 15 katika  kanda hiyo  kutakuwa na mchezo kati ya timu ya Super star Vs Turuka fc.

Na kanda ya Makata kuna jumla ya timu 4 zitazoshiriki ligi ya Alizeti cup ambazo ni Makata fc,Naiulu fc,Kigwema fc na Cristabela fc.

Mchezo wa ufunguzi unatarajiwa kupigwa agosti 18 kati ya timu ya Makata fc ikiwakaribisha Naiulu fc na agosti 19 kutakuwa na mchezo kati ya Kigwema fc dhidi ya Cristabela fc.

Post a Comment

 
Top