Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aonya vyama vya siasa kutumia maneno yanayovunja amani na usalama wa nchi.
Masaju
ambaye amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es
salaam leo, ametolea mfano Oparesheni UKUTA iliyotangazwa kufanywa na
CHADEMA na kusema kuwa ina maneno ya kijeshi yanayotumiwa kwenye
shughuli za kihalifu.
Amesema neno UDIKTETA siyo sahihi kwa kuwa nchini Tanzania hakuna
udikteta kwa kuwa serikali inafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria
na nchi inaendeshwa kwa kuzingatia mgawanyo wa madaraka wa katika
miimili yote mitatu ya dola.
“UKUTA lengo lake ni nini, ni sawa na kuwatenganisha wananchi na
serikali yao” Amesema Masaju na kuwataka wananchi kutambua kuwa Septemba
Mosi ni siku ya Majeshi nchini huku akishangazwa na CHADEMA kuchagua
siku hiyo kuzindua kampeni yao aliyodai kuwa ina lengo la kuvuruga nchi.
Masaju amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kutii mamlaka za
dola ikiwemo Jeshi la Polisi na mahakama iliyowapa mwongozo juu ya ombi
la kupinga zuio la jeshi la polisi na pia kufuata ushauri waliopewa na
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora juu ya kutokuwepo kwa udikteta
nchini.
Amesema sababu kuu za kuzuia Oparesheni ni mbili ambazo ni hali ya
usalama kutokuwa shwari, pamoja na kutokuwepo kwa udikteta nchini.
Post a Comment