0

 Manchester City imemsajili beki John Stones kutoka Everton kwa kitita cha pauni milioni 47.5 na kumfanya kuwa difenda wapili ghali zaidi ulimwenguni.

Stones, mwenye umri wa miaka 22, anayechezea timu ya taifa ya England, ametia sahihi mkataba wa miaka sita.


Mchezaji huyo alikuwa ametajwa kwenye orodha ya timu ya Manchester City ya wachezaji watakaoshiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, hayo ni kulingana na tovuti ya UEFA kabla ya makubaliano ya usajili wake kukamilika.

Stone amesema itakuwa vigumu kupata nafasi katika timu hiyo lakini atajitahidi kuwa mchezaji bora.
Stone alishiriki mechi 95 katika misumu mitatu aliyokaa Everton na aliwafungia bao moja kipindi hicho.

Post a Comment

 
Top