Utafiti unaonyesha
kuwa madaktari wa nchi za kusini mwa Afrika wanatoa dawa nyingi zaidi ya
zilizoagizwa na Shirika la Afya Duniani WHO.
Utafiti huo
uliofanywa na Chuo kikuu cha London kwa ushirikiano na kituo cha Kutoa
ushauri wa afya cha nchini Ghana,ikihusisha nchi kumi na moja za kusini
mwa jangwa la Sahara zinaonyesha kuwa wagonjwa wanapewa takribani dawa
tatu kila wanapotembelea hospitali, moja zaidi ya maelekezo ya WHO.Inasemekana tatizo ni baya zaidi kwenye taasisi zinazotengeneza faida, na kuchochea kuuza dawa.
Tafiti zimeonya kuwa matumizi makubwa ya madawa yanasababishwa na kulazimishwa kutumia dawa, kuzidisha dozi na kuleta athari mbaya kwa mchanganyiko unaosababishwa na kuchanganya dawa mbalimbali.
Pia wamegundua wagonjwa wengi wamekuwa wakipewa dawa za kutuliza maumivu pasipo kufanyiwa vipimo, na kuongeza hatari ya maambukizo yanayosababisha na kupambana na dawa.
Post a Comment