0


Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu amewatangazia kiama wauza pombe wakati wa kazi akisema  ataanzisha msako wa nguvu kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Nkurlu alisema vijana wengi badala ya kufanya kazi wanakimbilia kunywa pombe na kuvuta dawa za kulevya.

Wakati Nkurlu akipiga marufuku kitendo hicho, Umoja wa Wamiliki wa Baa na Nyumba za Kulala Wageni wilayani Kahama, umeunga mkono agizo la kufungua baa saa kumi jioni siku za kazi.

Mwenyekiti wa umoja huo, Julias Machage alisema agizo hilo ni la kitaifa na wanalikubali,alisema wamepokea barua kutoka Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ikiwataka kufunga baa wakati wa kazi.

Nkurlu alisema atawachukulia hatua wafanyabiashara watakaokutwa wanafanya biashara hiyo muda wa kazi.

Post a Comment

 
Top