Kocha wa timu ya
riadha ya Kenya inayoshiriki michuano ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro
amerudishwa nyumbani kwa kosa la udanganyifu.
Mkuu wa Timu ya
Olimpiki ya kenya, Kip Keino amesema John Anzrah aliigiza kama miongoni
wa wakimbiaji wa mita 800, na kutoa sampuli ya mkojo kwa niaba ya
mkimbiaji Ferguson Rotich.
Udanganyifu uligundulika na wakaguzi wa
dawa za kusisimua misuli baada ya kuangalia picha za kitambulisho
alichokuwa amevaa, ndipo walipogundua kuwa sura ya Bwana Anzrah
haeindani na mchezaji aliyefanya uchunguzi.
Mkuu wa Timu ya
Olimpiki ya kenya,Kip Keino amesema uongozi wa timu yake hautavumilia
tabia hiyo ingawa mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyotolewa dhidi ya
Rotich.
Anzrah ni afsa wa pili kutoka kenya kurejeshwa nyumbani,
Wa kwanza akirudishwa kwa kosa la kuomba rushwa ili kuweza kukwepa
upimaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Kumekuwa na idadi
kadhaa ya wanariadha wa Kenya ambao walishindwa kufuzu vipimo vya
matumizi ya dawa za kuongeza nguvu huku ni wiki iliyopita tu shirika la
kupambana na matumizi ya dawa hizo WADA likiiondoa Kenya kwenye nchi
zilizoshindwa kutimiza masharti.
Post a Comment