Rais wa jimbo la Jubaland nchini Somalia Ahmed Madobe
Mamlaka katika
jimbo la Jubaland nchini Somalia imetangaza kusitisha shughuli ya
kuwapokea wakimbizi wa Somalia wanaowasili katika eneo hilo kutoka
Kenya.
Shughuli ya kuwarudisha makwao wakimbizi hao kutoka kambi
ya Dadaab ilianza mwaka 2014,lakini imeongeza kasi mwaka huu baada ya
Kenya kutangaza kuwa inafunga kambi kubwa ya wakimbizi ya Dadaab.
Waziri
wa maswala ya ndani katika jimbo la Juba Mohammed Warsame Darwish
ameambia BBC kwamba wakimbizi hao wanakabiliwa na hatari zaidi kwa
sababu hawapati misaada ya kibinaadamu ilioahidiwa kwao wakati
watakapowasili katika maeneo yanayodhibitiwa.
Waziri huyo amelaumu
shirika la wakimbizi katika Umoja wa mataifa UNHCR kwa kutofuata
mipango iliowekwa na badala yake limekuwa likiwawacha wakimbizi hao
katika maeneo yanayodhibitiwa na mamlaka ya jimbo hilo.
Post a Comment