SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Walifanya jambo ambalo sikulitegemea kabisa, kama wangelifaya kwa upande wangu, ni vile walivyokuwa wakinitizama kwa dharau
kiasi cha kwamba , nilihisi uwenda kuna kitu nimekifanya kibaya dhidi yao,
lakini nikakumbuka si kuwa na wafahamu labda wao ndio walikuwa wakinifahamu.
Sikutaka kuisumbua akili yangu nilipuuzia, nikiongoza kule kwenye ofisi ya mkuu
wa chuo.
Lakini sasa
ofisi ilinipokea katika namna ya aina yake, macho yangu yaliweza kuona lile kwa
uzuri kabisa, ni kweli niliona.
***********
“Aahhh! nani tena?” , haraka nilijitoa ndani
kuelekea nje baada ya kusikia sauti ikiniita jina langu. Haikuwa ya mwingine, ilikuwa sauti ya mjomba.
Nilishangaa ujio wake katika mshangao ambao tayari nilikuwa na majibu nao.
“Karibu
anko”, nilimkaribisha kabla ya kumsalimu, wakati huo akikaribia ndani na kuketi
katika moja ya sofa. Punde mjomba aliniuliza habari za mama, nikamwambia yakuwa
ametoka kidogo, kauelekea kwenye mikutano yao. Hivyo alikubaliana nami na
maneno yangu, tuliendelea kukaa pale sebuleni wakati huo, nilikuwa nimempatia
maji kama alivyokuwa, ameniagiza.
Aliendelea kunywa taratibu huku kinywa chake kikionekana na mengi ya
kusema lakini, katika namna ambayo nilikuwa najua sipaswi kujua kutokana na
tabia yake mjomba.
Nilikuwa Kimya tu huku sauti ya runinga kidogo
ikifukuza kimya kile, kabla yakufukuzwa kwa mazungumzo yetu sasa, tulizungumza
sana na mjomba kwa wakati ule, mazungumzo ambayo mjomba aliyatawala sana. Ilikuwa
juu ya masuala yangu ya shule, hakuchoka kunisisitiza niendelee kusoma
iliniweza kufaulu mtihani wangu, huku akinipa mifano mingi mingi kuhusu maisha.
Nami nilikubaliana na maneno yake kwa kiasi kikubwa. Aliendea mbali zaidi na
kunikanya kuhusu mahusiano katika namna moja ama nyingine nami nilikubaliana
nae kabisa na hata asingeniambia habari za mahusiano kwa upande wangu moyo
wangu, haukuwa tayari kabisa kujihusisha ndani ya dhahama hiyo. Ni kweli tangia
hapo nyuma sikuwahi kupenda na kuhusu wanawake nilikuwa nikisikia tu kwa watu
na kamywe sikuwahi kujua uzuri wa viumbe hivyo zaidi ya mabaya ya viumbe hivyo
labda vingenifanya niwe mfuasi kama wa viumbe hivyo kama binadamu wengine.
Hivyo pale maneno yake mjomba kuhusu wanawake kwangu niliona hayana tija hata
kidogo.
Mazungumzo yetu yalianza kukatishwa na njaa
kali iliyoanza kuchachafya tumbo langu, japo nilijitahidi mwanzoni kujizuia
lakini hali ilionekana kuleta ugumu upande wangu. Nilijua wazi mama asingeweza
kurudi na kufikia kupika, hivyo ilinibidi niandae chakula cha haraka. Akili
yangu ikafikiria kwenda kuchukua samaki wa kukaanga ambao hawakuwa wanakaanga
mbali na maeno yale ya nyumbani. Nilivyomaliza
kutaarisha ugali. Nilichepuka haraka kwenda kuchukua samaki ambao niliona
wangefaa kabisa katika kuridhisha tumbo langu na hata la mjomba. Kuhusu mama
sikuwa na shaka nae mara nyingi hakienda kwenye vikao vyao huwa akirudi hanaga
mpango wa kula.
Kweli nilifanikiwa kuridhisha tumbo langu
baada ya dakika kama kumi, hapo walau maneno ya mjomba yaliweza kupenya vizuri
kwenye masikio yangu kwa mara nyingine kuliko hata awali. Wakati tukiendelea kuzungumza baada ya kumaliza
kula, haikupita muda mrefu hatimaye mama alirejea kutoka mkutanoni na kukuta
ujio wa mjomba machoni mwake.
Sidhani kama mama alikuwa anategemea mjomba
angekuwa pale kwa nyakati ile. Maana ilikuwa ajamaliza hata siku tatu alikuwa
amerejea tena. Mjomba alionekana ana mengi yakuongea katika kinywa chake.
Sikutaka kuendelea kukaa pale, baada ya
kuzungumza kidogo na mama huku akinipatia maagizo ya kwenda sokoni kwa muda ule,
alikuwa kama anajua kuwa nisingeendelea kukaa kusikiliza maongezi yao.
Taratibu niljitoa ndani, miguu yangu
ikiongoza soko lilipo, dakika chache tu zilinifanya nifike eneo lile, nilichukua
nilichokuwa nimeagizwa na kurejea nyumbani. Wakati huo nilikutana na maongezi
yalikuwa yakiendelea kati yake mama na mjomba, sikutaka kuyafatiria. Nilijitoma
ndani ya chumba changu baada ya kumkabidhi alichokuwa amenituma.
Nilijibwaga juu ya kitanda nikiwa katika
tafakuri kidogo, ni kweli tafakuri ile ilinitoa pale nilipokuwa na kunipeleka
mbali zaidi, katika namna ambayo sikudhani kama ingenipeleka mbali. Na kiri
wazi ndugu msikilizaji, mawazo ni kitu kibaya sana, hakika ni ubaya ambao uwezi
kuoona katika jicho la kawaida. Mwili
wangu ulikuwa pale kwenye kitanda lakini akili haikuwa pale kabisa, hata nusu
saa, lisaa linipita nikiwa pale pale juu ya kitanda, huku nikiwa nimeyakodoa
macho yangu juu tu.
Naikumbuka siku ile, ndio haikuwa imenipotea,
naam!. Mawazo ya shule yalinijia nikiwa kitandani pale. Haswa nilikumbuka siku ile, nilivyoletewa
habari za kupendwa na msichana, haikuwa kazi ndogo katika kutuliza mzuka wangu.
Hakuna aliyetegemea uwenda ningezipokea habari zile katika mtazamo wa namna
ile, mtazamo ulijaa chuki ndani yake. Na si hivyo tu aina ya msichana mwenyewe
ndio ilifanya watu wa nione wa ajabu kweli. Na kiri tena ndugu msikilizaji
alikuwa msichana ambaye hakuna mwanafunzi wa kiume wa shule yetu asingependa
kuwa nae, Mungu alikuwa amekijalia kiumbe hicho, mwili wa wastani, usiochukizwa
kwenye macho ya wapenda ngono. Lakini kwangu
hakupata nafasi walau kumtazama mara mbili mbili na kubadili msimamo
wangu. Ilikuwa bahati nzuri kwake siku
hiyo naweza kusema maana lilishia juu juu baada ya fikra zangu, kuamua
kulipoteze jambo lile, huku nikitoa onyo kali kwa msichana yule.
Sasa lilikuwa limejirudi jambo lile nikiwa
kitandani pale, akili yangu ilikubaliana yakuwa nilikuwa sahihi kabisa katika
lile, tofauti hata nilivyokuwa nikidhani. Nilisonya mara mbili kabla ya kuamka
na kutikisa kichwa changu, huku nikionya kisinilitee kumbukumbu ambazo hazikuwa
na faida kwangu.
Ni muda huo, ambao nilisikia sauti ya mama
ikiniita na mimi kujitoa ndani, kiuvivu kwenda kumsikiliza. Hakuwa na jipya
sana ilikuwa kama nilivyokuwa nikidhani ya kuwa ilikuwa nyakati ya kutumwa
tena. Ndio lazima ingekuwa hivyo maana hapakuwa na mtu wakumsidia kazi pale
nyumbani walau dhahama hiyo ya kutumwa tumwa isingekuwa kwangu. Nilijitoa
kusikiliza wito, katika nyakati ambazo tayari juu lilikuwa likielekea kuondoka
kwenye uso wa dunia.
Wakati huo macho yangu yalikutana na tabasamu
pana la mjomba kuliko kawaida, ni hilo tabasamu ambalo lilikosekana nadhani kwa
kipindi kirefu kwake. Macho yangu yalipigwa na kama bumbuwazi, kabla ya kukiri
sasa mjomba alikuwa ni yule ambaye niliyokuwa nimezoea, katika siku za nyuma.
Moyo wangu ulifarijika sana, nilitamani kuendelea kumwangalia lakini sauti ya
mama ilikuwa imeshapita ikiniagiza dukani kuendea chumvi.
*********
Siku hiyo ilikuwa tofauti sana, nilitegemea
ningeweza kurejea mapema nyumbani, kutokea dukani kwa Mangi, lakini nilikuatana
na wateja kadhaa ambao walikuwa na mengi mahitaji hivyo ilinisubirisha sana,
ubaya akili yangu hakunishungulisha kuliendea duka lingine, na pale
nilipokumbuka umbali wa kuendea duka lingine mwili wangu ulinyongonyea na
kuendelea kusubiria pale pale. Mvumilivu hula mbivu baada ya dakika kama kumi
hivi nilipata nafasi ya kuhudumiwa.
Nilirejea nyumbani, nyumba ilinipokea katika
namna ambayo sikuitegemea.

Post a Comment