Ndugu msikilizaji kwa jina naitwa
Criss Lugongo, asante sana kwa kunipa nafasi hii ya kusimulia simulizi hii ya
maisha yangu kwa ujumla. Hakika ita kuburudisha na kusisimua na bila kusahau
kujifunza katika mkasa huu mzito, niliaomua kuupa jina la TETEMEKO LA MOYO
Chanzo cha yote. .
Sasa tuanze nayo.
Ukumbi ulivutia katika namna
isiyoelezeka, kiukweli waandaji wa idara ya mapambo walifanya kazi yao ipasavyo.
Tofauti hata nilivyokuwa nikidhani. Hakika kulivutia katika macho ya kila mmoja
aliyekuwa amefika sehemu ile. Uzuri si idara ya mapambo tu iliyofanya kazi yake
ipasavyo la hasha kila moja alifanya kazi yake vile nilivyohitaji mimi na
mpenzi wangu Irene ndani ya siku ile. Katika siku ambayo Irene wangu, alikuwa
akitimiza miaka kumi na tisa. Ni hiyo miaka iliyotufanya tuwe pale kwa muda ule
kusherehekea pamoja na ndugu na jamaa wengine. Yote niliyafanya mimi kwajili ya
upendo wangu na thamani yake ndani ya moyo wangu. Iren kwangu alikuwa zaidi ya kila kitu. Muda mfupi
tangu uhusiano wetu ulipoanza, siku zote nilijitahidi kumfanyia mambo mazuri
yote kuonesha thamani yake kwangu kama wafanyavyo wanaume wengine kwa wenzawao.
Hakika sikuwahi kufikiriya ipo siku nitakuja kufikia katika namna hii ambayo
isiyoelezeka. Naichukia nafsi yangu, naiichukia sana.
_______
Siku hiyo ilipendeza sana, uzuri kila
moja aliyepata mwaliko alifika kwa wakati husika. Si wanafunzi wenzetu katika
chuo chetu si marafiki wengine kila moja alifika kwa wakati huku wakiwa wamependeza
kuliko kawaida. Hali ile ilinogesha sana siku hiyo, sijui niseme nini kwa
upande wangu nilikuwa na furaha isiyo elezeka. Nilionekana wazi kwenye taswira
ya uso wangu dhahiri, na hata kwa upande wa Irine ambaye aliyetufanya tuwe pale
muda ule naye alionekana mtu mwenye furaha kupita maelezo. Hakika hakuna
aliyetamani kuisha kwa siku ile, kila mtu aliyekuja pale alijisikia yupo sehemu
tofauti sana kutokana na hali ya ukumbi wenyewe. Kulipendeza sana, nakshi naskhi za mule ndani
ziliwavutia wageni waalikwa, walikula wakanywa vinywaji kila aina ya vyakula na
vinywaji walivyokuwa wanavipenda.
Siku hiyo ilikuwa ni muhimu sana
katika namna mbili, ya kwanza ilikuwa ni
siku yake ya kuzaliwa Irene wangu. Pili nilimvisha pete ya uchumba. Ilikuwa kwasababu upendo wangu nilihitaji
kila mtu ajue ni jinsi gani nilivyokuwa nampenda msichana yule kutoka ndani ya
moyo wangu nasi vinginevyo. Hakika nilikuwa nimepagawa sana na mwanamke yule
maana nilikuwa tayari kujitolea chochote kwajili yake.
Nakumbuka hapo awali sikuwahi kupenda
na sikuwa mshirika wa dhahama hiyo. Akili yangu haikuwa ikifahamu nini maana ya
mapenzi, nilikuwa nikiyangalia katika mtazamo usiokuwa na maana mbele ya kichwa
changu. Mtazamo uliloleta majibu mengi hasi tofauti na chanja kwa upande wangu.
Kila mtu aliyekuwepo alishuhudia tukio
lile kwa macho yake mawili, ijapokuwa kipato changu kilikuwa cha kati na hata
wazazi wangu ila nilijibana huku na huku. Kutimiza yote yale ndani ya siku ile.
Nilijichanga sana hatimaye nilifanikiwa kufanya yote yale bila mchango wa mtu
yoyote.
**********
Mwezi moja ulikuwa umepita tangu
yatokee yote yale nikiwa bado nipo kitandani nauguza majeraha katika mwili
wangu niliyoyapata muda mfupi tu baada ya kumalizika sherehe ya kipenzi changu
Irene. Niliumia vibaya sana sehemu za ubavuni kwenye zangu mbavu,
vile vile nilivunjika mguu hivyo, nilikuwa mtu wa kulala kitandani muda wote
mpaka sasa tangia ajari ile iliyosabishwa na dereva wapikipiki niliyoipanda
muda mfupi tu baada ya kuagana na Irine nilipoenda kumrudisha hostel.
Sasa yalikuwa yamejirudi katika kichwa
changu. Nikiwa kitandani, yaliongeza maumivu makali niliyasikia kwenye mwili
wangu. Maumivu ambayo hayakuwa tu yakisababisha na majeraha yale niliyokuwa
nimeyapa la hasha maumivu yalichanganyika na mateso ya moyo. Moyo ambao tayari
ulikuwa ushasalitiwa katika akili ya kawaida. Macho yangu hayakuweza kumwona
Irine kwa kipindi chote hicho, walau yangeweza teta na moyo wangu. Ilikuweza kuupa
faraja pindi yangemuona Irene. Namna
nilivyokuwa nimeyakumbuka yale yaliniumiza sana sikuamini juu ya yote yale
niliyomfanyia Irene katika siku si nyingi zilizopita.
Ameshindwa hata kunijulia hali hata
kwenye simu yangu. Maana kama kufika nyumbani kwetu ilikuwa tatizo hata hilo
ameshindwa baada ya wiki tu nilipopokea simu yake katika kile nilichoona
unafiki katika masikio yangu.
Uvumilivu ulinishindwa nilibanwa na
kilio cha chini chini ,nikiwa juu ya kitanda ambacho hakikuwa na hiyana kama
binadamu. kiliufariji mwili wangu kwa wakati wote. Lakini sasa kilishindwa
kunibembeleza katika kilio. Kilio kilichochanganyika na majuto ndani yake.
Hali yangu ilibadilika grafla mwili
ulikosa nguvu, nikajikuta mboni zangu zinapoteza taswira. Weusi ulitawala
katika vishimo vya macho yangu, masikio yalikuwa mazito sikuweza hata kujua
anayeingia wala anayetoka ndani ya chumba changu. Hata sauti bembelezi ya
kitoto ya mdogo wangu Criss haikupata tena nafasi kwa wakati huo. Ni huyo Criss
mdogo wangu mbaye mara nyingi hupenda kucheza karibu na kitanda changu. Katika
namna niliyokuwa nikiona ni faraja kutokana na hali yangu.
***********
Hata sikuelewa nipo wapi baada ya muda
ambao nilihisi ni mfupi baada ya kutokea hali ile. Nilishangaa nilipofumbua
mboni za macho yangu shuka jeupe
lilikuwa limeufunika mwili wangu huku kibaridi kwa mbali kilikuwa kinapenya
ndani ya mwili wangu, ulikuwa unatoa vimaji maji ambavyo dhahiri ilitokana na
hali nilikuwa nikisikia ndani ya mwili wangu. Niliangaza kidogo baada ya macho
yangu kuipata nuru kwa mara nyingine. Kichupa kidogo cha wastani kikiwa
kinaning'ing’inia juu ya kitanda kidogo tofauti na cha kwangu, ilitosha kabisa
kufahamu pale nilipo kwa muda ule, kwa
uhakika kabisa kuwa mahali pale kulikuwa
hospitali. Si kufahamu wakati
sahihi niliokuwa nimefika mahali pale na chanzo cha mimi kuwa pale. Nilijiuliza
maswali ambayo hayakuwa na majibu ya wazi kwenye kichwa changu, akili ilikuwa
bado imeganda kabisa. Wakati nikisubiri jibu nilihisi kama kitu kipo kwenye
mkono wangu. Kabla hata sijaangalia vizuri nini kipo mkononi mwangu, nilimuona
mama yangu akiwa anaongea na mtu ambaye kwa muonekano tu nilijuwa ni daktari.
Maongezi yao yalipenya vizuri kwenye ngoma za masikio yangu. Kwa uhakika kabisa
masikio yangu yalikuwa katika ubora wake. Ubora ambao ulipotea muda mfupi kabla
ya kuwa eneo lile. Daktari yule aliongea kitu ambacho kiukweli hakikuniingia
akili kabisa. Na si mimi hata mama yangu nilivyomuona nilibaini kuwa jambo lile
hakuwa anakubaliana nalo.
Si kuwa tayari hata kidogo kwa kile
kilichokuwa kinaendelea, nilijua wazi sasa ni muda wa mama kuangahika, huku
ikiwa si ya chini ya mwezi moja tu, pesa nyingi sana alitumia kwajili yangu hii
leo suala la kwenda India kwa jili ya uchunguzi wa moyo wangu. Lilikuwa geni
kabisa masikioni mwangu. Hapo awali sikuwahi kuugua maradhi ya moyo hata
kidogo. Na hata huku nyuma hakuna mtu ambaye ndani ya ukoo wetu ama familia
yetu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo. Hivyo juu ya kweli kwamba moyo
wangu huenda una matatizo kama daktari alivyoshauri, punde tu kabla hata
haijafika miezi sita liwe imepatikana ufumbuzi, tena nje ya nchi haikuniingia
akilini hata kidogo. Wakati huo nikiwa bado nitaendelea na dawa kwa jili ya
kupunguza maumivu yale kwa muda mfupi.
Ijapokuwa ni kweli nilihisi mabadiliko
muda mfupi kwenye upande wa kushoto wa kifua changu eneo sahihi ulipo moyo
wangu. Ila bado niliona hali iliyokuwepo mbele si nzuri hata kidogo. Nilitamani
kupingana na maneno ya yule daktari, lakini ni kaona ni sawa na ujinga tu. Ujinga
wa kupingana na mtu ambaye alikuwa akipambana na kuikoa afya yangu. Fikra zangu
zikaonekana kubaliana na lile kwa kinyongo . Ni kinyongo cha ambacho nilishajua
hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kutumia pesa. Hali yetu kiuchumi si kwamba ilikuwa mbaya
sana ila kidogo ingeleta shida kwa namna moja ama nyingine.
Nilitulia kimya kama vile nilikuwa
sijui jambo lolote liliokuwa likiendelea, ni kiwa bado nipo kitandani chumbani
mule, huku nikisikilizia maumivu makali ndani ya mwili wangu.
Pande zote zilivuta kuliko kawaida,
ila nilijikaza kiume si kutaka kuonesha udhaifu kama baadhi ya wagonjwa wengine
pindi wapatapo maumivu makali utawasikia tu, “hiiiiiiii... ohhooo nakufa!..mama
mie nakufa!..mara uwiii Mungu wangu nisaidie!”. Kwa upande wangu nilikuwa kimya
huku nikiwa nimeyafumba macho yangu kusikilizia maumivu kimya kimya.
Nilihisi mwili wangu ukiguswa guswa maeneo ya usoni kama baadhi ya watu wanavyofanyaga kupima hali ya mgonjwa. Nilifumbua macho yangu taratibu hayakuchelewa kuona mtu aliyekuwa akifanya vile. Hakuwa mwingine bali alikuwa ni mama yangu taswira yake ndani ya mboni za macho yangu ilitambulika vizuri. Sura yake ilionesha wazi ya kuwa alikuwa akipata maumivu makali kutokana na hali yangu.
"Pole Eddy utapona mwanangu",
nilimsikia vyema mama akiyatamka maneno yale ndani ya kinywa chake huku
yakifatiwa na mengine yakunitia moyo. Alionekana bayana kuwa ana mashaka na
hali yangu, wakati huo aliendelea kuongea maneno mazuri yakunitia nguvu.
Muda ulienda hatimaye kile kichupa cha
wastani kilichokuwa juu ya kitanda changu kilionekana kuishiwa maji. Ambayo
niliyaona ya kitiririka kuelekea katika moja ya mkono wangu huku yakiwa
yanapita kwenye kama kibomba chemba sana kuelekea ndani ya mwili wangu. Kupitia
tundu dogo lilotobolewa kwenye mkono wangu ikiunganisha sehemu ya juu ya
kichupa kile kuelekea kwenye wangu mwili kwa tararibu. Kadri yalivyokuwa yakienda
hali yangu ilianza kurudi kama mwanzoni kabla sijafikishwa eneo lile pale
nilipojikuta na kosa nguvu na nuru kupotea kwenye macho yangu. Lakini sikujua
kilikuwa kichupa cha ngapi?, ila mwenendo wake ulinirudishia nguvu zangu.
Jioni baada ya hali yangu kuonekana
kidogo imerudi sawa daktari hakuona haja ya mimi kuendelea kubaki alichofanya
nikutupatia ruhusa. Na kumpatia mama maelekezo pamoja na kumpatia dawa kwajili
ya matibabu yangu. Nilishuhudia mama yangu zikimtoka pesa nyingi sana, hapakuwa
namna yoyote yeye ndio alikuwa mtu pekee wa kuyatenda yale. Wakati ule ambao
hakukuwa na mtu ambaye angeweza kusaidiana bega kwa bega na mama katika ugonjwa
wangu . Baba ndio alikuwa mtu pekee ambaye angemsaidia mama katika hali ile
lakini alikuwa tayari ameshakufa katika miaka miwili iliyopita. Kipindi ambacho
hata nilikuwa sijamaliza elimu yangu ya kidato cha sita.
Mtu pekee katika familiya alikuwa ni
mama si kwamba ndugu hawakuwepo la hasha ilitokea hali ya kutoelewana baina ya
ndugu zake baba. Pindi alipofariki ilikuwa katika ile hali ya ndugu kutaka
kutudhurumu haki yetu kama watoto na pamoja haki yake mama kama mke wa
marehemu. Baada ya zoezi la kurithi mali za baba kutatuliwa na mahakama ndipo
uhusiano wetu ulipovunjika. Na kwa upande wa ndugu zake mama hali zao zilikuwa
ni za chini na kiasi kikubwa walimtegemea mama yangu kwa kila kitu.
__________
Wiki tu baada ya kuruhusiwa
hospitalini hali yangu iliendelea kuimalika siku hadi siku majeraha nayo
yalianza kupona, huku nikiwa chini ya uangalizi wa mama. Alihakisha na kula
vizuri na pata dawa kwa wakati, miezi mitatu ilipotimia majeraha yote yalipona
kabisa huku yakiniachia makovu sehemu za mwili wangu, kama kumbukumbu. na kwa
upande wa moyo wangu ulitulia kabisa naweza kusema zile dawa zilinisaidia
kabisa.
Kwa kipindi chote kile si kuweza kupata
habari yoyote iliyomhusu Irene hata nilipowasiliana na baadhi ya marafiki zangu
hawakuwa wananipa taarifa zake. Nilijua wazi wananificha ila sikutaka kufatiria
sana kutokana na hali yangu ilivyo. Ukizingatiwa mama kipindi chote nilipokuwa
najiuguza aliniambia daktari ameshauri nisiwe mtu wa mawazo muda wote. Ingeweza
kunisabishia madhara ndani ya moyo wangu. Na kingine zaidi alichokuwa
akisisitiza ni suala la kuwa mbali na mambo ya mapenzi yangechangia sana
kunifikirisha na kujikuta anapata upinzani mkali kutoka kwenye moyo wangu.
Hivyo nilijaribu kuepuka sana jambo lolote linalohusisha mawazo ndani ya kichwa
changu kabisa. Ijapokuwa Irene alikuwa akinijia sana ndani ya kichwa changu
katika namna isiyoelezeka.
************
“Criss... Criss....Criss!”, nilisikia
vizuri sauti ya mama ikiwa inanita ikitokea nje wakati nikiwa bado nikiwa
naendelea kusoma kitabu kile kilichoandikwa na Kaka miaka kadhaa. Niliiumia sana, huku bado nikiwa na shauku
maisha ya kaka yalikumbwa nanini na kwanini Kaka aondoke kipindi ambacho
nahitaji msaada wake kwajili ya maisha yangu?. Niliendelea kujiuliza maswali
wakati huo sauti za mama zilizidi kupenya kwenye ngoma za masikio yangu.
Nilificha haraka haraka kijitabu kile ili hata kama mama akija asijue nilikuwa
nafanya nini ndani. Niliona sehemu sahihi ni chini ya kitanda. Nilikiweka
haraka na kutoka nje.
SIMULIZI MARIDHAWA. TETEMEKO LA MOYO
NA MWANDISHI. YONA FUNDI.
MAWASILINO :0675278759.
NA MWANDISHI. YONA FUNDI.
MAWASILINO :0675278759.
NA KURUSHWA HEWANI NA LIWALE BLOG
Post a Comment