0

Wanachama wa chama cha wananchi CUF mkoani Mtwara wamewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wanaotarajiwa kukutana August 21 mwaka huu kumkubalia aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahimu Lipumba arejee kwenye nafasi yake ili kukiimarisha chama hicho.

Wamesema tangu Prof.Ibrahimu Lipumba atoke kwenye nafasi ya Mwenyekiti, chama hichi kimekuwa kikiyumba ambapo wamesema hakuna wa kusimamia na kukemea mambo mabaya yanayotokea ndani ya chama hicho.

Ni katika ufunguzi wa shina la chama cha wananchi CUF katika mtaa wa Chipuputa manispaa ya Mtwara mikindani ambapo ndipo imeibuka hoja ya kuwataka wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na baraza kuu kukubali Prof. Lipumba arudi katika nafasi yake ya uenyekiti na kwamba  wamesema kukosekana kwa kwakekatika nafasi hiyo pigo kwa chama hicho kwani hakuna wa kukemea mabaya yanayofanyika ndani na nje ya chama.

Katibu wa CUF mkoa wa Mtwara Said kuraga amesema katika tafiti waliyoifanya kwa kipindi kifupi ndani ya mkoa wa Mtwara wamebaini kuwa wanachama wengi wanamtaka Pro. Lipumba arejee kwenye nafasi yake ili kukiimarisha chama huku mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Maftaha Nachuma anasema anaungana na wananchama wake waliompa ridhaa ya ubunge.

Post a Comment

 
Top