0


Jeshi la polisi limesitisha leseni za madereva 18 wanaoendesha mabasi yanayofanya safari zake kuanzia manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwenda mikoa mbalimbali walioshiriki kufanya jaribio la mgomo kutoa huduma kwa lengo la kushinikiza mahakama kuwaachia madereva wenzao waliokamatwa kwa makosa ya mwendo kasi.

Akizungumza kwenye kikao cha pamoja baina ya jeshi hilo na Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA jijini Dar es Salaam kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga amesema wakati jeshi la polisi likichukua hatua hiyo imewataka wamiliki mabasi hayo kuchukua hatua mara moja kwa waajiriwa wao kwani kitendo cha kufungiwa leseni zao wanakuwa wamepoteza sifa ya kuajirika.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu SUMATRA Gilliard Ngewe amebainisha kuwa tangu mwezi novemba mwaka jana sumatra ilibadilisha adhabu kwa madereva wanaoendesha kwa mwendo kasi kwa kuwafikisha mahakamani badala ya kuwatoza faini ili mahakama itoe maamuzi hivyo amewataka wamiliki wa mabasi kujieleza kwa nini madereva wao wasifungiwe leseni zao kutokana uvunjaji wa wazi wa kanuni za leseni za usafirishaji na kuwachukulia hatua mara moja ili iwe fundisho kwa wengine.

Aidha amezitaja kampuni zinazomiliki mabasi hayo kuwa ni RS express, kimotco, princes muro mabasi mawili, osaka raha, bunda express, vislam bus, sabuni exp. premier line, masaba royal class, Ngasamo na Ncheye classic.

Post a Comment

 
Top