0


POLISI mkoani Singida inamtafuta mtu mmoja aliyewahi kuwa Mganga Msaidizi Vijijini (RMA) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mzee wa miaka 70 baada ya kumfanyia upasuaji wa tezi dume.

Inadaiwa kuwa RMA huyo ambaye alikuwa mwajiriwa serikalini miaka mingi iliyopita, alifanya upasuaji huo Julai 14 mwaka huu akiwa hana ujuzi, utaalamu wala vifaa vya kufanyia shughuli hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka, mtuhumiwa huyo Joseph Msafiri (40) ni mkazi wa Kijiji cha Kinyambuli, wilayani Mkalama mkoani hapa ambaye alimfanyia upasuaji Israel Shaban (68) mkazi wa kijijini hapo.

Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kugeuza nyumba yake kuwa kituo cha kutolea huduma za afya, alimchukua mzee huyo hadi nyumbani kwake kisha akamfanyia upasuaji wa tezi dume, hata hivyo mzee huyo alipoteza maisha muda mfupi baada ya kutokwa damu nyingi.

Kamanda Sedoyeka alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuona hivyo, alitoroka na kutokomea kusikojulikana.

Post a Comment

 
Top