Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akisaini kitabu cha
wageni katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambapo alifanya ziara ya
kikazi ya siku nne na kutembelea maeneo
mbalimbali ya hifadhi ya Hifadhi ya Misitu na Wanyamapori yenye
migogoro. Maeneo hayo ni Hifadhi ya Msitu wa Wembere (Wilaya ya Igunga),
Eneo la Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima (Wilaya ya Kaliua), Eneo la Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole (Wilaya ya Skonge), Msitu wa Hifadhi wa
Ipembampazi (Wilaya ya Skonge) na Msitu wa hifadhi wa Ilomero (Wilaya ya
Nzega).
Naibu
Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani akizungumza na baadhi ya wananchi
waliovamia Msitu wa Hifadhi wa Wembere Wilayani Igunga hivi karibuni.
Aliwataka wananchi hao kutii sheria za nchi na kusubiri maelekezo ya
Serikali ambapo aliwaagiza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga na
Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kukusanya taarifa mbalimbali
zinazohusu hifadhi hiyo na vijiji jirani ambapo zitatumika kumaliza mgogoro huo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa waliovamia Msitu wa Wembere na kuweka makazi,
Wilayani Igunga hivi karibuni. Alitoa maelekezo mbali kwa viongozi wa
Halmashauri ya Wilaya na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania kwa ajili ya
kukabili changamoto zilizopo katika hifadhi hiyo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na Viongozi
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Igunga pamoja na viongozi
wengine kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto)
akikagua maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Isawima Wilayani Kaliua hivi
karibuni. Hifadhi hiyo ambayo imetengwa na vijiji 11 kwa ajili ya
kuanzishwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima umevamiwa na
wananchi kutoka maeneo ya nje ya vijiji hivyo na kuweka makazi, mifugo
na kilimo jambo lililoikwamisha jumuiya hiyo kupewa kibali cha
kurasimishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii. Eng. Makani alitoa maelekezo
kwa uongozi wa Wilaya ya Kaliua na Halmashauri kutumia mamlaka ya kisheria
waliyo nayo kuwahamisha wavamizi hao ili jumuiya hiyo iweze kuanzishwa.
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua wakiwa kwenye
Mkutano wa Hadhara wa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Mtapenda, Wilayani Kaliua alipotembelea kuona
changamoto wa Uhifadhi na kuweka utaratibu wa kuzikabili.
Mmoja
wa wananchi waliovamia Hifadhi ya Isawima, Kaliua, Charles Msinda
(kulia) akiiomba Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Maliasili, Eng.
Ramo Makani (wa pili kulia) iwafikirie kuwapa maeneo mbadala baada ya
kuondoka katika Hifadhi ya Msitu huo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati) akizungumza
na viongozi wa Chama (CCM) na Serikali Wilayani Skonge. Kulia kwake ni
mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na jamii wa
wavuvi wa Mto Koga, Wilayani Skonge ikiwa na hatua ya kusuluhisha
mgogoro kati yao na muwekezaji, Muhsin Abdllah "Shein" ambaye ni
Mkurugenzi wa Northern Hunting. Eng. Makani aliwataka viongozi wa Wilaya
na Halmashauri kukaa pamoja na muwekezaji huyo na wadau mbaimbali kwa
ajili ya kamaliza mgogoro huo. Aliwata viongozi hao kuangaliwa upya
vibali vinavyotolewa kwa wavuvi hao ili idadi yake ilingane na ukubwa na
mahitaji ya Mto huo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akisikiliza
malalamiko kutoka kwa muwekezaji ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Northern Hunting, Muhsin Abdallah (kushoto) aliyewekeza katika kitalu
cha uwindaji kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ipole Wilayani
Skonge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ipembampazi,
Wilayani Skonge Tabora. Wananchi hao wameiomba Serikali iwamegee eneo
la hifadhi kwa ajili mradi wa kilimo cha umwagiliaji, Uluwa, Hifadhi ya
Msitu ambao upo chini ya Halmashauri ya Wilaya Kaliua. Eng. Makani
alitoa maelekezo mbalimbali kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya na
Mkoa ikiwa ni pamoja kuangalia taratibu za kisheria na kimazingira juu
ya uwezekano wa ombi hilo na kuliwasilisha Wizarani kwa ajili ya hatua
zaidi. (Picha na Hamza Temba - WMU - www.wizarayamaliasilinautalii. blogspot.com)
Post a Comment